Najibu kulingana na elimu yangu ya udaktari wa wanyama maana mie sio daktari wa binadamu hivo naomba nisiulizwe maswali yoyote yanayohusu swala zima la corona.
Mwilini mfumo wa kupambana na vimelea umegawanyika katika makundi mawili ambayo ni defence line ya kwanza na defence line ya pili, vimelea vinapofanikiwa kupita ngome ya kwanza ambayo immune cells ambayo ndio first line ya defence ya mwili, hao vimelea (pathogens) wanataenda kukutana na second line of defence ambayo inaundwa na B-cells na T-cells
Hawa B-cells wao wanadeal na kuzalisha askari kinga wa kupambana na infection ambazo zinaweza kuwa za bacteria au virus au wengine, ambapo waga wanaenda kuundwa specific kulingana na aina ya ugonjwa (antibodies)
Na huyu T-cells amegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Helper T-cells na Killer T-cells, ambapo huyu Helper T-cells yeye anaenda kusaidiana na B-cells kwenye zoezi zima la kutengeneza Antibodies lakini huyu Killer T-cells yeye anaenda kuuwa zile Cells za mwili ambazo zinakuwa zimeathiliwa na ugonjwa husika
sasa baada ya kuugua na kupona ndipo hizi cells kwa pamoja yani B-cells na T-cells zinaunda Memory ya pathogens ambao walishambulia mwili wakati uliopita ili kama wakija kwa mara ya pili basi wasiwe na kazi ya kurudia process bali ni kuzalisha moja kwa moja Antibodies
Lakini tunajua kuwa virus wana sifa ya kubadirika badirika nawewe wakati unaugua na mwili unaunda Antibodies waliunda dhidi ya strain fulani na sio zote, kwahiyo kama utakuja kuwa infected na corona tena kwa mara ya pili ambao watakuwa sawa sawa na wale wa awali maana yake mwili wako utakuwa na Natural vaccine ambayo iliundwa wakati umeugua kwa mara ya kwanza
Lakini kama ikitokea umeugua corona lakini ikawa imekuja na strain au aina tofauti ya virus safari hii mwili wako hautakuwa na Natural vaccine ambayo itapambana na hao virus kwa 100% na hapo ndipo linakuja swala la kutakiwa kupewa tena chanjo ya corona maana hujui exactly watakuja wajuba wa cuba au Alshabab. Nadhani kwa huu uelewa wangu mdogo angalau nimejaribu kujibu mkuu
Sent from my M2101K7AG using
JamiiForums mobile app