msaboi2020
Member
- Jun 20, 2020
- 11
- 9
KATIBU WA MKOA CHAMA CHA MAPINDUZI,
S. L. P. 19989
DAR ES SALAAM 22/07/2020
Ndugu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam,
Husika na kichwa cha Habari.
Kwa heshima kubwa sisi wagombea ubunge Jimbo la Ukonga, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam; kwanza tunakupongeza kwa kusimamia taratibu, kanuni na Sheria zinazotawala katika chama chetu tangu ulipoteuliwa. Ndugu Katibu Mkoa, sisi ni baadhi ya wagombea tuliokuwa tukiomba ridhaa kutoka kwa wanachama wenzetu kupeperusha bendera ya chama kwa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es salaam, tunaleta malalamiko kwako kuhusu ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi.
Malalamiko yetu ya msingi yapo katika maeneo haya:
1. Idadi ya wajumbe waliohudhuria kikao cha uchaguzi kuwa tofauti na idadi iliyotarajiwa (hii ilifanya mwenyekiti wa mkutano kuwaomba wajumbe wasiokuwa na sifa kuondoka kwenye kikao hicho). Wilaya haikujua wapiga kura wake halali.
2. Kuruhusiwa kupiga kura kwa baadhi ya wajumbe wasiokuwa na sifa za kupiga kura. Miongoni mwa wajumbe hao ni pamoja na Nashoni Kiweru Mwenezi wa tawi la Kilimo Kata ya Gongolamboto, Marwa Chacha wa Kitunda na baadhi kutoka kata ya kivule; ambao walisimamishwa kwa tuhuma mbalimbali
3. Kupungua kwa karatasi za kupigia kura kitu kilichofanya zaidi ya wajumbe sita (6) kukosa fursa ya kupiga kura mpaka wakapewa karatasi zingine. Wakati wa zoezi la kupiga kura fomu za kupigia kura zilikwisha na kusabisha kusimama kwa zoezi hilo kwa zaidi ya nusu saa bila maelezo yeyote.
4. Tukiwa tunaendelea na uchaguzi, zaidi ya wajumbe hamsini waliondoka ukumbini bila ya taarifa. Baadhi ya wajumbe na wagombea walipohoji meza kuu ilijibu kwamba wamekwenda msikitini kuswali. WASIWASI WETU NI KWAMBA MEZA KUU ILIJUAJE KUWA WAJUMBE WALIOTOKA NJE BILA RUHUSA KUWA WAMEENDA MSIKITINI? Wasiwasi wetu ni kwamba meza kuu ilijuaje watu walioondoka bila ruhusa kwamba wanakwenda kuswali msikitini? Aidha kule msikitini lilikuwa ni chimbo la rushwa (liliratibiwa na Ojambi (cashier wa Jerry ) Frank Mangati na Imelda) maana wajumbe walikuwa wanapewa pesa ndani ya msikiti kitu kinachofanya viongozi wa CCM wilaya kuhusika moja kwa moja na zoezi hili.
5. Wajumbe kutolewa nje ya ukumbi ili kurahisisha kuingizwa kwa wagombea haramu na kuwatafutia ushindi baadhi ya wagombea.
6. Baadhi ya wagombea na wajumbe kuruhusiwa kuingia ukumbi wa mkutano wakiwa wamechelewa kwa zaidi ya masaa ya nne kupita tangu mkutano kuanza.
7. Vitendo vya wazi vya rushwa kwa baadhi ya wagombea miongoni mwao wakiwemo Ndugu Jerry William Slaa, Mohamed Msofe, Robert Masegesa, Tickey Ndile Kitundu.
a. Usiku wa kuamkia uchaguzi yaani tarehe 20/07/2020 makatibu wote wa kata wa jimbo la Ukonga waliitwa na Ndugu Jerry William Slaa katika Ofisi za kata ya Ukonga na kupewa kiasi cha Tzs 200,000/= kwa kila mmoja.
b. Pamoja na Wilaya kugharamia usafiri kwa wajumbe wote bado Mgombea mmoja Ndugu Jerry William Slaa alitoa magari ya usafiri kwa kata zote. Ndani ya daladala hizo wajumbe walikuwa wanapewa fedha kiasi cha Tsh 50,000/= wakati wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano.
c. Kulikuwa na gari la Jerry William Slaa ndani ya eneo la ukumbi wa uchaguzi ambalo lilikuwa linatoa fedha kwa wajumbe wa mkutano kiwango cha kuanzia Tzsh 50,000/= hadi 200,000/= kwa kila mjumbe. Kuna vidhibitisho vya jumbe za meseji ambazo zilitumwa kwa baadhi ya wajumbe kuwashawishi kwenda kuchukua fedha kwenye gari hilo. Pia kwenye kwenye vyoo vya nje vya ukumbi ambao uchaguzi ulikuwa unafanyika kulikuwa na kulikuwa kunagawiwa fedha kati ya Tsh 20,000/= na kuendelea zilizotolewa na Tickey Kitundu, Mohamed Msofe na Robert Masegesa. Aidha kuna ushahidi wa wazi wa namba 0744910258 ya wakala iliyokuwa inatuma fedha kwa wajumbe wa mkutano kama rushwa
d. Pamoja na kuwa na vyoo ndani ya Ukumbi bado wajumbe waliruhusiwa kutoka nje ya ukumbi kitu kilichokuwa ni chanzo cha vitendo vya rushwa kwani baadhi ya wajumbe walikuwa wanapewa fedha vyooni.
e. Baadhi ya wajumbe walishonewa sare za vitenge na wagombea ambao ni Robert Masegese na Mohamed Msofe. Miongoni mwa kata zilizoshonewa sare ni pamoja na kata ya Kipunguni, Pugu stesheni na Majohe. f. Wajumbe waliopewa pesa walilazimishwa kuhakikisha wanapiga picha ya kila karatasi ya kura na kutuma kwa WhatsApp kama kithibitisho kwamba wamempigia kura za ndiyo mgombea Ndg. Jerry Slaa na Robert Masegesa. Hiki kilifanya Mwenyekiti wa kikao kutoa tamko la kuzuia watu kupiga picha kura husika dakika chache kabla ya zoezi kumalizika; hii inadhihirisha kwamba viongozi walikuwa wanajua mapema nini kinachoendelea.
8. Kutokuwa na Imani na viongozi wa CCM wilaya ya Ilala hususani Mwenyekiti, Katibu na wasimamizi wa uchaguzi katika kura za maoni wa jimbo la Ukonga kwani walionyesha vitendo vya dhahiri vya kuwabeba baadhi ya wagombea.
a. Baadhi ya wagombea walitajwa majina yasiyokuwa ya kwao. Mfano Mgombea Ndugu Mwashabani Mrope alitajwa majina yasiyokuwa yake kwa zaidi ya mara nne. Ila pamoja na kukosea kwa majina hayo bado Mwenyekiti hakuonyesha dhamira yeyote ya dhati kuhusiana na hilo. (Ikumbukwe kuwa Mwenyekiti wa CCM ILALA ANAFADHILIWA NA JERRY SLAA).
b. Mfano mwingine ni siku ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu tarehe 17/07/2020 ambapo baadhi ya viongozi wakuu wa CCM Wilaya na wenyekiti wa kata walimbeba kwa lazima Ndugu Lamesh Patel kwenda kumchukulia fomu ya kuomba kugombea udiwani na walivyochukua fomu hiyo wakamjazia kwa kuomba nafasi ya Ubunge badala ya udiwani lakini waliandikisha na kulipia kwa Tsh 10,000/=. Baada ya hapo walimbeba mpaka wilayani wakaenda kumchukulia fomu ya kugombea Ubunge na pale walipofika wakapewa fomu na aliyekuwa ameachiwa ofisi pamoja na malipo yake ya Tsh 100,000/= kwa sababu wasingerudisha fomu bila risiti ya malipo halali.
9. Kuna zaidi ya wagombea hamsini (70) walikuwa wamepandikizwa na Ndg. Jerry Slaa ambapo aliwalipia fedha za kuchukua fomu wagombea wenzetu kwa makusudi ya kutawanya kura wakati hawakuwa na nia ya kugombea. Kuna ushahidi wa wazi kabisa kwamba ndugu Jerry Slaa aliwaita baadhi ya wagombea siku ya tarehe 19/07/2020 ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ikiwemo kuishawishi meza kuwapa upendeleo wa aina yoyote ile katika zoezi zima la kupiga kura na kuhesabu. Kikao kiliratibiwa na Ndugu Fatma Komba wa Ukonga Mazizini, Yusuph Hokororo katibu mwenezi wa Chanika pamoja na Hassan Jalala ambaye ni katibu mwenezi kata ya Gongola Mboto.
10. Ndugu Katibu, siku moja kabla ya uchaguzi na tulipoingia ukumbini kabla ya maelekezo yoyote yale tulishangaa wapambe wa Robert Masegesa, Tickey Kitundu, Mohamed Msofe na Jerry Slaa walianza kuwapokea wajumbe na kuwapa namba na majina ya kuwapigia kura wakati wagombea wote hawakuwa wakijua namba zao ambazo zilitolewa baadae wakati wagombea, wajumbe na watu wengine waalikwa walipofika ukumbini. Baadhi ya wagombea waliwasiliana na Wilaya lakini waliambiwa namba zitapatikana ukumbini. Ndugu Katibu hii ilitupa picha kwamba wagombea hao wenzetu Usiku wa kuamkia upigwaji wa kura walikutana na watendaji hao ambao waliwapa karatasi za kupigia kura hivyo wakawapa wapambe wao wawaeleze wajumbe hata kabla hawajafika ukumbini.
11. Pamoja na kasoro hizo lakini pia karatasi za kura ambazo awali ilitarajiwa ziwe na picha zetu za wagombea lakini hazikuwekwa na hivyo kuharibu kabisa zoezi hilo kwasababu baadhi ya wajumbe waliwatambua wagombea kwa sura. Ndugu Katibu, kutokana na mwenendo uliojitokeza wa upigaji kura za maoni hadi sasa yafuatayo yamejitokeza:
1. Wengi wa wajumbe hawana Imani na mchakato mzima wa uchaguzi mpaka matokeo.
2. Kuna viashiria vya wazi wazi vya baadhi ya vyombo vya kulinda haki kama TAKUKURU kuhusika moja kwa moja kumbeba mmoja wa wagombea Ndugu Jerry Slaa. Hii ni kwa sababu gari la taasisi hilo limekuwa likionekana maeneo mengi wakati mgombea huyo akiwepo pia katika eneo husika. Mfano gari hilo lilionekana Pugu Kajiungeni karibu na ofisi za Kata ambapo Ndugu Jerry alikuwa ndani ya ofisi hiyo akiongea na viongozi wa Kata wa jimbo la Ukonga. Mfano wa viashiria vingine ni kwamba gari linalosemekana kutumika kutoa pesa pale ukumbini lilikaa mkabala na gari hilo la TAKUKURU. Pia kuna baadhi ya wajumbe walijaribu kuongea na watu wa TAKUKURU kuhusiana na waliyoyaona pale nje ya ukumbi na msikitini lakini wale watu hawakuonyesha jitihada zozote za dhati kitu kinachoonyesha kwamba kulikuwa na mpango kabambe wa utekelezaji wa tukio hilo.
3. Wagombea wanakosa Imani na viongozi wa ngazi zote pamoja na mstakabari wa jimbo letu kwani uchaguzi huu umeharibu taswira nzima ya Chama kwani wanachama wa Jimbo la Ukonga wamekosa Imani na uongozi wote wa CCM ngazi ya Wilaya (Katibu Idd Mkoa, Mwenyekiti Ubaya Chuma pamoja na Mwenezi SABABU WAMEONEKANA KUWABEBA BAADHI YA WAGOMBEA WATOA RUSHWA) na baadhi ya viongozi wa Mkoa.
Pia TUNASHAURI KUWA VIONGOZI WALIOTAJWA HAPO JUU WASIHUSIKE KWENYE VIKAO VYA MAAMUZI KWANI HATUNA IMANI NAO kwani mwaka 2015 jimbo lilikwenda upinzani na hizi pia sio dalili nzuri sana.
Mwisho Ndugu Katibu, tunaomba zoezi hili la uchaguzi lifanyiwe uchunguzi wa kutosha ili wagombea wote waliokiuka taratibu za uchaguzi washughulikiwe kulingana na taratibu za Chama Cha Mapinduzi kwasababu tunauhakika kwamba walioshika nafasi za juu hawakupata kura hizo kihalali.
WAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA KWATIKETI YA CCM, 2020.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Nakala:
1. Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi.
2. Makamu Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi.
3. Katibu Mkuu Chama cha Mapinduzi.
4. Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam.
5. Afisa Usalama wa Mkoa Dar es salaam.
6. Afisa Usalama Kanda ya Ilala.
7. Mkurugenzi Mtendaji- Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa -TAKUKURU.

YAH: UKIUKWAJI WA TARATIBU ZA UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA, DSM