Habari wana bodi,
Hii ni shule ya serikali inayosimamia na TAMISEMI iliyopo Jiji la Arusha. Sisi wazazi na jamii nzima tunaelewa na tunapewa elimu mara kwa mara na mamlaka mbalimbali za serikali kama vile TRA juu ya ulipaji wa kodi na kudai risiti na tunatambua pia kuwa ktk shule hizi za serikali michango iliyokubaliwa lazima ilipwe kwenye akaunti ya shule.
Cha kusikitisha na kushangaza katika shule hii ya mrisho gambo sekondari, tunalipa fedha mkononi (cash) na kwenye simu ya mwalimu na hakuna risiti!
Hii shule ina mabweni yaliyokamilika ambayo yalijengwa kwa fedha zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Arusha. Sasa sharti la mtoto kupata nafasi ya kulala kwenye haya mabweni lazima awe amelipa michango ifuatayo;
1. TZS 700,000/= kwa mwaka kwa ajili ya hosteli
2. TZS 200,000/= kwa ajili ya kitanda na hizi fedha zimekuwa zinatolewa na mzazi anayehamishia mtoto kwenye hii shule tangu mwaka juzi 2023 lakini hakuna kitanda kinachonunuliwa.
3. TZS 100,000/= kwa ajili ya dawati kwa mwanafunzi anayehamia toka shule nyingine.
Utaratibu wa malipo ya TZS 700,000/= zinalipwa nusu kwa mwl mkononi anakuandika jina na hakuna risiti au unaingiza kwenye namba yake ya simu ambayo ni 0712-473481 na nyingine ya voda.
Utaratibu wa malipo ya TZS 200,000/= na TZS 100,000/= zinalipwa mkononi kwa Mkuu wa shule anakuandika jina hakuna risiti. Hivi kwa wanafunzi 500 ni kiasi kikubwa cha pesa kukusanywa kienyeji bila kupitia kwenye akaunti na zinatumika bila kufuata taratibu za manunuzi.
Hivi serikali ipo macho kweli kwa shule ambayo ipo mjini katika mkoa ambao unasemwa una mkuu wa mkoa mchapakazi? Ina mbunge mchapakazi tena shule ina jina lake? Wizara zinazohusika zichukue hatua ama shule zote nchi nzima ziruhusiwe kufanya hivyo.