hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 13,628
- 20,992
ANDIKO LA MSINGI
Yohana 1:43-46. Biblia inasema hivi:
"43. Siku ya pili yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate. 44. Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro. 45. Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. 46. Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone."
Ni muhimu kufahamu kuwa Nazareti ulikuwa ni mji mdogo uliokuwa kusini mwa jimbo la Galilaya (Lower Galilee). Mji huu ulikuwa miongoni mwa miji iliyodharauliwa sana. Kwa ujumla, Israeli ilikuwa na majimbo makuu matatu:
1. Yuda
2. Samaria
3. Galilaya
Yuda liliheshimika sana kwa sababu lilikuwa eneo lililotoa manabii na viongozi wakubwa walioonyesha utii kwa Mungu. Lakini Galilaya na Samaria hayakuwa maeneo yenye heshima kutokana na historia zake za:
Kuwa na ibada za sanamu
Watu wasioshika dini
Viongozi waovu na wasiomcha Mungu
Kwa sababu hizi, Galilaya ilidharaulika na kuonekana kama mji usioweza kutoa neno jema.
Nazareti na Unabii wa Masihi
Kwa mujibu wa unabii wa Agano la Kale, Masihi alitarajiwa kutoka Yuda, haswa katika mji wa Daudi – Bethlehemu.
Mika 5:2 inasema:
"Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele."
Hii ilithibitishwa pia katika Mathayo 2:1-6, ambapo mamajusi walikuja kuuliza:
"Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia."
Hata wakuu wa makuhani na waandishi walithibitisha kuwa Masihi atazaliwa Bethlehemu ya Uyahudi.
Kwa Nini Nathanaeli Alihoji Kuhusu Nazareti?
Kwa msingi wa mafundisho ya kiyahudi, ilikuwa vigumu kwa Nathanaeli kuamini kuwa mtu aliyetabiriwa na Musa na manabii angeweza kutoka Nazareti.
Kwa ujumla, Nazareti ulikuwa mji usioheshimika, uliosifika kwa:
Umasikini mkubwa
Mmomonyoko wa maadili
Watu wasiomcha Mungu
Waabudu sanamu
Nazareti haikuwahi kutajwa katika unabii wa Agano la Kale. Wakati huo, mtu akitoka Nazareti alionekana sawa tu na mtu anayetokea maeneo ya kawaida yasiyo na heshima, kama vile: Mbagala, Gongo la Mboto, Manzese, Kwatango, Kilosa, Mbulizaga (Pangani), Kwa Msisi (Handeni), Nchebebwa (Newala) au Naluleo (Liwale).
Katika Yohana 7:40-42, 52, tunasoma jinsi maadui wa Yesu walivyotumia mji wake kama njia ya kumdharau.
www.facebook.com
Mathayo na Unabii wa Nazareti
Mathayo 2:19-23 inaonyesha kuwa Mathayo alijaribu kuonyesha kuwa kuna unabii kuhusu Yesu kuitwa Mnazareti.
Hii inahusiana na Isaya 11:1, ambapo neno "shina" au "chipukizi" kwa Kiebrania ni "Netser", ambalo linafanana na jina Nazareti.
Mafundisho Muhimu kutoka kwa Somo Hili
✔ Mungu anaweza kuinua mtu kutoka hali ya kudharaulika.
✔ Ingawa Nazareti ilikuwa mji mdogo na usio na heshima, jina lake lilipounganishwa na Yesu Kristo, likapata umaarufu mkubwa duniani.
✔ Yesu alikubali kuitwa Yesu wa Nazareti.
✔ Majini na mapepo yalipotajiwa jina la Yesu wa Nazareti, yaliogopa na kutoka kwa nguvu.
✔ Mitume walipotenda miujiza walilitumia jina la Yesu Kristo wa Nazareti.
✔ Leo hii, mji wa Nazareti ni maarufu kwa sababu ya Yesu Kristo.
Mtu akipokea Yesu Kristo, maisha yake hubadilika kabisa. Haijalishi unatokea ukoo gani, kabila gani, au jamii gani, ukiunganishwa na Yesu, historia yako inabadilika. Hata kama ulikuwa mnyonge kiasi gani, Mungu anaweza kukuinua na kukutumia kwa njia ya ajabu.
Filipo
alimwambia Nathanaeli:
"Njoo uone!"
✅ Mtu akiunganishwa na Yesu, maisha yake yanabadilika!

Bei Facebook anmelden
Melde dich bei Facebook an, um dich mit deinen Freunden, deiner Familie und Personen, die du kennst, zu verbinden und Inhalte zu teilen.