Ukiwa huna hela unakuwa kama mjinga mjinga hivi hata sauti inabadilika


Kujiamini ni kitu kikubwa sana. Life is all about confidence and how you express yourself.
 
Hahahaa umenichekesha sana ,ila kwangu huwa naamin ,bila kujalisha mazingira nayokumbana nayo, sitokaa niishi chini ya magoti yangu.
 
Aiseee hahahaaa acha utani bwanaaa mwanaume anakuaje na sauti ya kike ghafla bin vuuu....kisa tuu no money lol,.[emoji23]

Ila kama chemchem ya furaha yako ni pesa wallah barabarani utaongea na upepo,.
Sweetheart
 
Mfano nikiwa na hela hata njaa siihisi na sikondi
 
mie ndio mashine haisimami kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Hahaaa umenikumbusha kipindi tupo o,level tulienda kwenye mgahawa mmoja baada ya mwezetu kupata boom la wazazi na kututoa out tulikuwa tunapiga kelele kias kwamba wahudumu walituomba mara kadhaa tupunguze sauti kimbembe kilikuja baada ya jamaa kukaribishwa mjini (aliibiwa pesa yote) kwenda mfukoni hola tena na tena hola wavulana wazima(kipindi hicho) tulitukanwa na kasichana kadogo kalitukana sanaaa tulitamani tugeuke kobe tuingize vichwa ndani kilichotuokoa jamaa yetu mmoja alikuwa na simu tukamwambia tuiweke simu bond tukitumiwa maboom tuje tuikomboe nashukuru mama yake na kale kasichana ambaye alikuwacashier aliipokoa sjui adhabu yetu ilikuwa ni nn sijui ata mybe tungeosha vyombo asee.
Kila mmoja alitoa sauti nyembaba kama inachujwa na filter ya sigara
 
Ukipambana kwa bidii hukosi ya kula na matibabu hebu tupambane kwasana
 
Silaha nyingine ya mzungu hiyo, inawatandika wengi kwa kila jinsia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…