Ukiwa konda lazima uwe chizi maarifa?

Ukiwa konda lazima uwe chizi maarifa?

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
6,373
Reaction score
16,073
Nawauliza nyie vijana wa DAR na sehemu zingine nchini [lakini haswa DAR], hivi ukiwa kondakta wa daladala lazima akili ziwe fyatu?

Sijawahi kukutana na konda msafi, wengi wao wanavuta mabange, wanavaa maguo yaliyoraruka na wanaongea kibabe kama wako vitani?

Huwezi kukutana na konda akakuongelesha kwa staha, ni lazima akufokee huku anakurushia mate usoni mpaka unajutraa. Hata kama jambo dogo tu, ni utafokewa mpaka.

Sasa nawauliza nyie wapanda daladala na vijana wa DAR, hili swala limekaaje ati? Kuna sheria labda ambayo inasema ukiwa konda lazima uwe chizi mwenye dishi lililoyumba?

Ukienda Ulaya napo unakutana na makonda wa aina hii tulionao Tanganyika?
 
Unamaanisha mpaka wale makondakta wakike au..!?
Em ongezea nyama hapo, juu ya hao pia.
 
Wafue saa ngapi...hawana mapumziko...
Saa kumi alfajiri to saa nne usiku..lazima akili ziyumbe..
 
umeharibu hapo mwisho, eti ukienda ulaya napo unakutana na...


Achana na ulaya jikite na mada tutafute njia zetu za kuwanyoosha hawa makonda.
 
Nlishaona konda na abiria wakizabuana kisa shingi 50,abiria akatoa mia 400 konda kakaza nauli 450,abiria akatoa jero akataka arudishiwe 50 yake konda kasema hana chenji,ukiangalia hapo ni kichaa ana deal na kichaa tuzoeane.
 
Nlishaona konda na abiria wakizabuana kisa shingi 50,abiria akatoa mia 400 konda kakaza nauli 450,abiria akatoa jero akataka arudishiwe 50 yake konda kasema hana chenji,ukiangalia hapo ni kichaa ana deal na kichaa tuzoeane.
😂😂😂😂😂🙌
 
Back
Top Bottom