Ukiwa mfanyabishara kaa mbali na makundi ya kisiasa

Ukiwa mfanyabishara kaa mbali na makundi ya kisiasa

Moto wa volcano

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
1,148
Reaction score
2,815
Ukiwa mfanyabishara Afrika /Tanzania kaa mbali sana makundi ya kisiasa usioneshe kufungumana na upande wa chama chochote au mtu yeyote .

Nchi zetu hizi za kiafrika bado utawala wa kidemokrasia haujakomaa kama nchi za wenzetu ambazo unaweza hata ukawa mfanyabishara wa makampuni mbali mbali na ukaonesha kumpinga au kutokumuunga mkono rais wa nchi na bado ukawa huru kuendesha shughuli zako bila vikwazo vyovyote

Kipindi Elon Musk anamuunga mkono mgombea wa chama pinzani Donald Trump , Rais alikuwa bado ni Biden lakini sikusikia bwana Elon akifanyiwa finigisu zozote

Kwa sisi wa Afrika sidhani kama tumefikia level hizo . Kwahiyo kwa mfanyabishara wa Afrika sishauri kuonesha ushabiki wa kisiasa
 
Kwa sisi waafrika ni kosa kuwa upande wa pili kuikosoa serikali, utafilisiwa, uchanganyikiwe, ujirushe ghorofani.
 
Back
Top Bottom