Ukiwa mtumishi wa umma usipoiibia serikali ili ujenge mjengo mkali, ununue gari kali na kufungua biashara wananchi wanakudharau

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hao ndio Watanzania, ukiwa mtumishi wa umma wanatarajia wakuone umepark ndinga kali kali uani mwako, uwe na mjengo wa haja , vimichango vya misiba na sherehe unatoa parefu hapo ewaaah watasema una akili bila kujua malipo yako halali ni Shilingi ngapi.

Hao hao baadaye wanasema nchi imejaa mafisadi huku watumishi waadilifu au watumishi wasiopata mwanya wa wizi wanawadharau kuwa wako serikalini lakini hawana maajabu.
 
Kumbuka yale mashirika ya mkoa (RTC) wakati wa mwalimu, wajanja walichota na kuwa matajri mpaka leo ni matajiri.
 
Mimi binafsi channel ya minoti haijanikalia sawa, nikipata fursa wala silembi napiga moja la mshindo na kutulia, Wazalendo walikuwa zamani akina Samora, Kaunda na wenzao!
 
Hao ndio Watanzania, ukiwa mtumishi wa umma wanatarajia wakuone umepark ndinga kali kali uani mwako, uwe na mjengo wa haja , vimichango vya misiba na sherehe unatoa parefu hapo ewaaah watasema una akili bila kujua malipo yako halali ni Shilingi ngapi.

Hao hao baadaye wanasema nchi imejaa mafisadi huku watumishi waadilifu au watumishi wasiopata mwanya wa wizi wanawadharau kuwa wako serikalini lakini hawana maajabu.
Tatizo la ubadhirifu katika Nchi yetu linaendekezwa na mtazamo katika jamii. Kwa mtazamo wa kuwa lazima ujitajirishe ukiwa kwenye Ofisi za umma inarudisha nyuma maendeleo kwenye Nchi yetu. Kuna haja ya kuongeza juhudi kutoa elimu ya uraia kuanzia shule za awali ili kuondokana na mtazamo huo.
 
Back
Top Bottom