Ukiwa mwanachama wa CCM ni raha tu. Ila ukiwa upande wa pili ni suluba tu

Ukiwa mwanachama wa CCM ni raha tu. Ila ukiwa upande wa pili ni suluba tu

kahembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2015
Posts
317
Reaction score
400
Kufanya siasa ukiwa CCM ni raha na rahisi sana tu ila sasa nenda upande wa pili yaani upinzani especially Chadema. Utajuta kwanini umechagua upande huo. Taabu na subili vyote ni vyako.

Polisi, kuumizwa, kupotezewa muda, kuharibiwa uchumi wako, kuonekana wewe ni gaidi, hayo yote kuwa tiyari kuyabeba.
 
Inaonekana hatupo tayari kuruhusu mfumo wa Vyama vingi/kuwa na mawazo mbadala ya kutusogeza mbele kama Taifa

Nilikuwa nawaza ikiwezekana turudie mfumo wa Chama kimoja
 
Hakika hatukua tayari kuwa na mfumo wa vyama vingi. Sijui wanapata raha gani kuwatesa watanzania wenzao na kuwaua
 
Hakika hatukua tayari kuwa na mfumo wa vyama vingi. Sijui wanapata raha gani kuwatesa watanzania wenzao na kuwaua
Bara walio wengi walikataa vyama vingi. Visiwani ilikuwa kinyume chake. Watawala wakasema vyama vingi vimekataliwa. Nyerere akasema umefika wakati wa kuwa na vyama vingi.
Watawala wakatekeleza matakwa ya Nyerere kinadharia tu. Sheria za kuhakikisha CCM itaendelea kutawala zikapitishwa. Hata ofisi ya msajili wa vyama ikaundwa ikiwa dhumuni lake kuu ni kudhibiti vyama vya upinzani.
 
Back
Top Bottom