Ukiwa mwanasiasa hakikisha unatenga muda wa kusoma na kuwaelewa wana falsafa wa enzi. Ni hitaji muhimu la maamuzi utakayofanya

Ukiwa mwanasiasa hakikisha unatenga muda wa kusoma na kuwaelewa wana falsafa wa enzi. Ni hitaji muhimu la maamuzi utakayofanya

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Asikudanganye mtu hakuna chochote kigeni kwenye hii dunia. Mambo yanayotokea leo hii yalishakuwepo kwenye huu ulimwengu miaka maelfu kwa maelfu iliyopita.

Unaongelea kuhusu rushwa, chuki, wivu, ukatili, ukabila, upendeleo, kulewa madaraka, magonjwa, mauaji etc etc yote utayakuta kwenye vitabu vitakatifu na ni vitu vilikuwa vinatokea kwenye karne zote za ulimwengu huu.

Maana yake, matukio yote ya sasa kwenye maisha tunayoishi, asilimia kubwa ni marudio tu ya mambo yaliyokwisha kutokea zama za nyuma.

Lakini kuna kitu kimoja watu huwa wanakipuuza, katika zama za enzi zilizopita, kumebarikiwa kuwa na watu wenye akili ambazo ni vigumu sana kuzipata kwenye watu wa dunia ya sasa ya kidigitali.

Akili hizi na maarifa ya wanafalsafa wa enzi, ndizo haswa zilizowezesha jamii za karne hizo kuweza kushindana na madhila na changamoto ambazo zilikuwa zinawakabili, kama ki siasa, kiuchumi, kijamii, kivita, kiteknolojia, kidini n.k

Maana yake ni kwamba Ukitaka kujifunza chochote kwenye ulimwengu wa sasa, fanya kurejelea maandiko ya wanafalsafa wa miaka ya zamani. Na huko ndiko busara ya kuchanganua maisha na changamoto za jamii itapatikana.

Ni kwanini, leo watu wanamuimba Nyerere ni kiongozi bora, ni simply kwa sababu nyerere alikuwa msomi mzuri wa falsafa.

Sikiliza hotuba zote za Nyerere kwenye masuala ya uchumi, halafu nenda kasome kazi za wanafalsafa wa uchumi akina Adam Smith, David Ricardo, au John Keynes.. utagundua anapita mule mule.. Ni kama vile alikuwa anachukua masomo ya wanafalsafa na kuyaleta kwenye applicability ya uchumi wa Tanzania..

Na hapo ndipo Nyerere alifaulu, kusoma kazi za wanafalsafa na kuzi apply kwenye content ya Tanzania. Sio kwamba Nyerere alikuwa Mungu mtu.. No.

*****

Hakuna mtu anayezijua vema falsafa, akachukua kiboko akamtandika mwenzake hadharani. Ukisoma vema falsafa, utakutana na maandiko ambayo daima yatakufanya uwe mtu mwema sana kwenye jamii, na mtu mwenye mawazo mema na ya busara.

Juzi kati hapa nilikuwa namsoma mwanafalsafa mmoja anaitwa 'Rene Deskates' kuna quote yake moja inasema "Greatest minds are capable of greatest vices and also of greatest virtues" kwa kiswahili ni kwamba, ' Watu wenye uwezo mkubwa wa kiakili wana uwezo wa kufanya matendo mema na pia wanauwezo wa kufanya ukatili wa kutisha.

Mstari kama huo hapo juu unaweza kumfanya kiongozi kuwa mpole sana wakati wote anapo deal na raia wake, maana huwezi jua huyo unayemnyanyulia fimbo kumchapa ni mtu wa aina gani na anauwezo wa kukufanya kitu gani.

Mambo kama hayo, yenye ufanano huo. Ni kukumbushana tu. Kuzijua falsafa ni kitu cha lazima sana kwa viongozi na wote ambao wana deal sana na jamii.

Wanafalsafa wenyewe ni wale kama kina Plato, Aristotle, soma Bible pia, Quran, Karl Max, wapo mamia kwa mamia, just tenga mda uwe unawasoma hao watu.

Na wamegawanyika makundi makundi.. kuna wanafalsafa upande wa uchumi, dini, siasa, sanaa, saikolojia, mahusiano ya jamii, sayansi, hisabati.. n.k ni wewe tu kuchagua wapi pa kuanza.. lakino kila mmoja utayemsoma lazima ujifunze kitu kipya

Kuna saa huwa nakaa natafakari, najisemea mwenyewe, watu kama kina Magufuli, Makonda, Sabaya na wengineyo, wangekuwa ni viongozi bora sana ikiwa wangezifahamu vyema falsafa.

Hakuna mwanafalsafa atayekushauri kufanya mabovu waliyofanya. Hakuna.

Nahisi kama ingekuwa ni amri yangu, qualification ya kuwa mwanasiasa, ingepaswa kwanza iwe mtu una degree ama cheti cha kwamba umesoma falsafa.

Ni hayo tu.
N. Mushi
 
Sio wanasiasa tu, hata raia wa kawaida ili wawe na ushiriki wenye tija katika michakato ya kidemokrasia lazima wawe wasomi wazuri wa vitabu.
Naam... na huu ndo usomi wenye kuleta tija.. ndio ilipaswa kuwa maana ya elimu.. kusoma vitabu vya wanafalsafa na kutatua changamoto za maisha hivyo tu
 
Kwenye hili la "degree", mimi sijui.

Kwa sababu mimi siku zote siamini ktk "vyeti vya shahada [degree] au Stashahada [diplomas] za vyuo au vyuo kikuu" kama kipimo cha ufahamu na uelewa wa mtu hata astahili kupewa uongozi.

Mimi ningependeza kuwepo na mfumo tofauti kabisa wa kupima uwezo na ufahamu wa mtu ili kumpa uongozi wa kitaifa unaoathiri maelfu ya RAIA bila ku - ignore education qualification ya mtu kama sifa ya ziada.

Yesu Kristo alikuwa ni mtu [binadamu]. Hakuwahi kwenda shule yoyote ya mfumo rasmi. Lakini mpaka leo huyu ndiye THE GREATEST LEADER OF ALL TIMES tangu kuumbwa kwa ulimwengu huu!

Kubwa lililompa sifa hii, NI UTII na UADILIFU WAKE KWA MUUMBA wake yaani YEHOVA. Hii yapaswa kuwa sifa kuu ya mtu yeyote anayetaka kuwa kiongozi Wa watu.

Kwa kujisomea tu na usomi wa falsafa, kwa sasa tunaye mtu mmoja tu kwa maoni yangu. Huyu si mwingine ila ni Tundu Antipas Lissu...

Huyu jamaa ni mtu wa kipekee sana. Ni mtu mwenye ufahamu na uelewa mkubwa sana wa mambo ya kidunia [global issues]. Nadhani ni kwa sababu ya kusoma sana
 
Huwezi kuona wachangiaji wengi hapa, but trust me umeongea moja ya jambo la maana Sana ambalo mwalimu Nyerere alilipigania Sana wakati anang'atuka madarakani na wakati wa ustaafu wake.

Maarifa mengi yamefichwa vitabuni, chochote ambacho unamkwamo nacho,ukitafuta vitabu vinavyoendana na ishu yako utapata ufumbuzi.

Tusome vitabu,tusiamini sana vyeti vya ngazi mbalimbali za elimu.
 
Mengine Sawa yalikuwepo zamani, lakini sio kila kitu, Facebook, Instagram, simu janja, train za umeme, Artificial intelligence, Computer, wimax, hotspot nk, hivi havikuwepo kipindi Cha Nuhu, Yesu, Ibrahim,Wala Mtume Muhamed S.A.W,
 
Mengine Sawa yalikuwepo zamani,lakini sio kila kitu,Facebook,Instagram,simu janja,train za umeme,Artificial intelligence,Computer,wimax,hotspot nk,hivi havikuwepo kipindi Cha Nuhu,Yesu,Ibrahim,Wala Mtume Muhamed S.A.W,
Ndo mana nikasema asilimia kubwa... nikimaanisha kuna ambavyo vipo sasa havikuwepo zamani..

lakini lazima uelewe hata hii artificial intelligence unayoiona sasa ni zao la wana falsafa wa zamani, watu kama akina Tesla, Newton, Shrodinger, Edison, Da Vinci etc.. bila kazi zao usingeona huu ugunduzi wa sasa
 
Jambo kubwa sana. Lkn Mungu katuonrsha wapi tulijikwaa na katuoa somo. Cha ajabu atakuja kuinuka jiwe mwingine akaingia ikulu tena miaka ya hivi karibuni. Ajabu kweli.
 
Huwezi kuona wachangiaji wengi hapa,but trust me umeongea moja ya jambo la maana Sana ambalo mwalimu Nyerere alilipigania Sana wakati anang'atuka madarakani na wakati wa ustaafu wake.
Maarifa mengi yamefichwa vitabuni,chochote ambacho unamkwamo nacho,ukitafuta vitabu vinavyoendana na ishu yako utapata ufumbuzi.
Tusome vitabu,tusiamini sana vyeti vya ngazi mbalimbali za elimu.
Yap mkuu hicho ndo cha muhimu.. ila hata kama mtu ni mvivu wa kusoma vitabu sahivi kuna google unaweza ukawa unapiga mdogo mdogo article mbalimbali za ma philosophers wa zamani
 
Ndo mana nikasema asilimia kubwa... nikimaanisha kuna ambavyo vipo sasa havikuwepo zamani..

lakini lazima uelewe hata hii artificial intelligence unayoiona sasa ni zao la wana falsafa wa zamani, watu kama akina Tesla, Newton, Shrodinger, Edison, Da Vinci etc.. bila kazi zao usingeona huu ugunduzi wa sasa
Mwambie akasome kazi za Da Vinci alafu atake the bow kwa jamaa.
 
Kwenye hili la "degree", mimi sijui.

Kwa sababu mimi siku zote siamini ktk "vyeti vya shahada [degree] au Stashahada [diplomas] za vyuo au vyuo kikuu" kama kipimo cha ufahamu na uelewa wa mtu hata astahili kupewa uongozi.

Mimi ningependeza kuwepo na mfumo tofauti kabisa wa kupima uwezo na ufahamu wa mtu ili kumpa uongozi wa kitaifa unaoathiri maelfu ya RAIA bila ku - ignore education qualification ya mtu kama sifa ya ziada.

Yesu Kristo alikuwa ni mtu [binadamu]. Hakuwahi kwenda shule yoyote ya mfumo rasmi. Lakini mpaka leo huyu ndiye THE GREATEST LEADER OF ALL TIMES tangu kuumbwa kwa ulimwengu huu!

Kubwa lililompa sifa hii, NI UTII na UADILIFU WAKE KWA MUUMBA wake yaani YEHOVA. Hii yapaswa kuwa sifa kuu ya mtu yeyote anayetaka kuwa kiongozi Wa watu.

Kwa kujisomea tu na usomi wa falsafa, kwa sasa tunaye mtu mmoja tu kwa maoni yangu. Huyu si mwingine ila ni Tundu Antipas Lissu...

Huyu jamaa ni mtu wa kipekee sana. Ni mtu mwenye ufahamu na uelewa mkubwa sana wa mambo ya kidunia [global issues]. Nadhani ni kwa sababu ya kusoma sana
Nimekulewa sana mkuu.. maana yake ni kwamba ni lazima mtu aoneshe kwamba ana uelewa fulani wa falsafa.. najua kabisa cheti ni makaratasi...
 
Na kitabu kizuri Cha kusoma pia ni Cha 48 laws of power by Robert Greene ni best kitabu kinachofundisha skills nyingi za ku attain power na kingine ni Laws of Human nature by Robert Greene
Kabisa.. 48 laws of power ni kama mkisanyiko wa masomo mbali mbali ya philosophers wa zamani..
 
Kwa taarifa, mkuu, "dictactor", ni cheo cha juu zaidi alitunukiwa mtawala, enzi za himaya kuu ya Rumi, mfano Julius Caesar.
 
Back
Top Bottom