Ukiwa mwizi halafu ukaoka, ukitoa ushuhuda huo wa kukiri hadharani haukamatwi?

Ukiwa mwizi halafu ukaoka, ukitoa ushuhuda huo wa kukiri hadharani haukamatwi?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Nimesikia kuna mtu anasema hadharani na wengine wanamsema wazi pia alikuwa mwizi kibaka anaibia watu mtaani ila sasa hivi katulia zake anatafuta riziki kwa njia halali.

Mtu wa aina hii hatakiwi kukamatwa na Polisi kupelekea mahakamani kushitakiwa?
 
Kazi ipo ngoja na mimi nitapeli tapel nikiokoka kupata mali nasema nampenda yesu
 
Ukimpeleka mahakamani unauthubitisho...?
 
Nimesikia kuna mtu anasema hadharani na wengine wanamsema wazi pia alikuwa mwizi kibaka anaibia watu mtaani ila sasa hivi katulia zake anatafuta riziki kwa njia halali.

Mtu wa aina hii hatakiwi kukamatwa na Polisi kupelekea mahakamani kushitakiwa?
Unakuwa umesamehewa dhambi tayari
 
Wasabato ndo zao kutoa ushuhuda mara alikuwa mwizi mara alienda chini ya bahari
 
Mtu wa aina hii hatakiwi kukamatwa na Polisi kupelekea mahakamani kushitakiwa?
Shitaka lazima liwe na MSHITAKI, vilevile na ushahidi usio na shaka. Ndipo anaweza kutiwa hatiani.

Otherwise ataruka kimanga na kusema hajasema hayo.
 
Utamshitaki Kwa reference gani mkuu? Kwamba ametamka kuwa alikuwa mwizi.. Je amesema aliwahi kumuibia nani pia? Je ametaja mali alizowahi kuiba pamoja na Sehemu alipoiba?
 
Shitaka lazima liwe na MSHITAKI, vilevile na ushahidi usio na shaka. Ndipo anaweza kutiwa hatiani.

Otherwise ataruka kimanga na kusema hajasema hayo.
Mshitaki wa makosa ya jinai ni Jamuhuri.
Hawezi kuruka kimanga hajasema hivyo kwa sababu kuna rekodi ya video clip.
 
Kwa hiyo hata mtu akiwa mbakaji akiacha ubakaji akawa anasema hadharani hivyo hakamatwi?
Ukimkamata itakubidi uithibitishie mahakama pasipo kuacha shaka yoyote kwamba alimbaka nani, alimbaka wapi, na upeleke vielelezo kama nguo zenye shahawa za mtuhumiwa
 
Kwa hiyo hata mtu akiwa mbakaji akiacha ubakaji akawa anasema hadharani hivyo hakamatwi?
mbakaji ni neno mtambuka, yaani mtu alikuwa anabaka huyu anabaka yule au inakuwaje? Neno mbakaji linatumika tu pale mtu huyo amekamatwa na kushtakiwa,vinginevyo huyo mtu anaitwa mzinzi. Na ni halali kuyasema maneno hayo kanisani kwa vile yuko ndani ya nyumba ya kuabudiwa,akitoka, akiyasema maneno hayo anakamatwa kwa upelelezi.
 
Kwa hiyo hata mtu akiwa mbakaji akiacha ubakaji akawa anasema hadharani hivyo hakamatwi?
Jinai haifi bro endapo ikithibitika pasi na Shaka kama alifanya uhalifu huo hata kama ni miaka 50 imepita anatiwa nguvuni.
 
Back
Top Bottom