Ukiwa na hela unaanza kuona kuweka kava la simu kama ushamba

instagram

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,118
Reaction score
4,863
Nina mda sasa natumia simu zangu bila kuweka kava yani inafika wakati naona kama kuweka kava ni ushamba flani.

Imagine watu wamekaa Apple huko wame design product yao wamekubaliana na muonekano wake wameamua kuachia kitu na raia wamekielewa alafu anakuja mtu anaweka kava yani inaondoa mantik nzima ya design ya simu.

Zamani nilikuwa na woga kwamba nikitumia simu bila kava itachakaa mapema lakini nimegundua kuwa hata simu ikiwa na kava pia inachakaa so nikaona kuweka kava ni dalili ya umaskini nikaachaga.

Sikuhizi nikiona mtu kaweka simu kava namuona kama wale wabibi wa zamani wanaonunua kochi alafu wanaweka vitambaa ili kochi lisichafuke au wale wabibi wa marekani wananunua kochi kisha wanafunika na kava la plastic ili lisichakae.

Kama unapenda bidhaa enjoy kama ilivyo. Nikiona mtu ana kava kwenye simu namuona kama mtu aliyetoka kijijini yani wakuja

 
Simu yangu ya mwisho nimekaa nayo miaka minne, nikaamua kuiacha baada ya betri yake kuchoka kabisa.

Siku naitoa kava na screen protector ilikuwa kama mpya kabisa wakati ndio ishachoka betri, baada ya kununua nyingine sijaweka kava wala screen protector nafurahia design yake kama ilivyotoka kiwandani.
 
Mimi simu,kava kama kawa na sina mpango wa kuacha karibuni unayeona ushamba ni wewe na hakuna aliyekuladhimisha kuweka.
 
Uko sahihi jombaa, kuweka kava ni mambo ya kishamba sana
 
Ss kava,pesa na ushamba mbona havina uhusiano?
Life s full of choices kwann uone watu washamba kisa ww kitu hukipendi?

Kila mtu anaweka Kwa sbb zake
Wengine mazingira ya kazi waliyonayo,kava,protector inasaidia sn hata cm ikianguka haipati madhara makubwa...
Wengine hasa wadada,urembo tu nk
Mkuu hayo ni mawazo yako tu,usiwapangie watu maisha
 
ukiona bado unatumia vifaa kujitangaza una pesa,mfano kuvaa nguo za gharama,saa kali,simu unaacha uchi ujue bado hujazikamata.

wenye mpunga wa kwenda wanaakuwa na majina makubwa mpaka wao ndio wanatangaza bidhaa,yaani eron musk kuonekana na iphone ni mchongo kwa apple.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…