Ukiwa na hela unaanza kuona kuweka kava la simu kama ushamba

Na sie mafundi mechanical tusiweke cover babu
 
Mimi lazima niweke cover kwasababu sipendi kushika simu nikasikia ule usoft.lakini pia simu ni yangu mambo ya muonekano yananihusu mwenyewe sio mtu mwingine.
 
Mimi acha tu nionekane mshamba
Kava naweka kwasababu huwa naiangusha hovyo na kuilinda na vumbi kutokana na mishemishe zangu.
 
Wewe unaongelea upuuzi gani sasa elon musk wawe wangapi? Nimesema ukifika level unaona simu si kitu cha kuhangaika nacho yani unakiwaza mpaka unakiwekea ulinzi kana kwamba kikifa hutapata tena huwezi ukahangaika na makava. Angalia watu wengi ambao kutoa hela kununua simu ya million 3 siyo ishu mara nyingi simu zao hata hazina kava wala glass protector yani hawazi itaharibika au itachakaa atashindwa kuiuza, yeye simu ikipasuka ananunua tu nyingine tena haendi yeye anampa dereva hela akamnunulie.

Ni sawa na mtu mwenye hela ya mawazo akipata hela ya kununua gari atanunua toyota kisa anahofia gharama za spea, ila waliovuka kiwango cha kuwaza spea za gari huwa wananunua tu gari yoyote iwe benzi au bwm bila kuhofia spea kwakuwa washavuka level ya kuhofia gharama za spea kwa kuwa wanazimudu.

Lakini then simu umenunua imetengenezwa na finishing nzuri ya titanium, aluminium na glass unaenda kuifunika na maplastiki ya bei nafuu.
 
Unahisi uko sawa???
 
Mimi kwa uzoefu wangu wa kuweka kava kwenye zimu zangu zilizopita nimegundua yafuatayo.

Cover zinatunza vumbi na uchafu hasa kwenye kingo za simu.

Cover zikiingia mchanga mdogo mdogo unasagwa baina ya mgongo wa simu na cover hali inayosababisha michubuko kwenye mgongo wa simu ( back)

Baadhi ya cover zinababua mgongo wa simu unaonekana kana madoa ya sabuni ya unga.

Cover zinasababisha joto na kuongeza uzito wa simu,

Cover hazizuii kioo kupasuka,wapo wenye cover na simu ina crack kama zote.

Cover inasababisha usiuze sura[emoji3][emoji3],wenye infinix na samsung galaxy mnakuwa na muonekano sawa.

Usipotumia cover ukiweka simu mfukoni inajisafisha yenyewe,ukitoa inakuwa smart kabisa.

Kama kazi yako ni mazingira machafu iweke pembeni sehemu laini ili usichubue mgongo.

Mimi simu natumia mpaka miaka mitatu na isidondoke hata mara moja,simu zangu zinapasuka crack baada ya kuichoka miaka mitatu hivi nakuwa careless.
 
Ni kweli kabis kava zinaweza fanya simu ikaoza na fangas kabisa. Umeeleza vema kuna vumbi zikiingia ndani ya kava zinachubua mgongo mimi nilishangaa mbona naweka kava alafu simu inachubuka? Siweki kava sikuizi, simu ya million+ kava elfu10?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…