Ukiwa na kipaji usikate tamaa, Push mpaka kieleweke

Ukiwa na kipaji usikate tamaa, Push mpaka kieleweke

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Kuna dogo alikuwa anajiamini kuwa na kipaji kikali cha kurap. Ndoto yake ilikuwa ni kuja kuwa staa mmoja mkubwa sana nchini Marekani na duniani kwa ujumla.

Hakujua ni kwa namna gani angetoka, akawa anafanya muziki wake chumbani kimyakimya, anatengeneza beat na kufanya ngoma kivaykevyake.

Siku moja akiwa kwenye mitikasi yake kitaa, akapita kwenye studio moja, akasikia ndani alikuwemo Shawn Carter ama Jay Z kama mnavyomjua. Dogo kusikia hivyo akarudi home fasta kuchukua cd iliyokuwa na ngoma zake.

Akarudi pale na kuambiwa mzee baba bado alikuwa ndani. Walinzi wamejaa mlangoni, hakujua ni kwa namna gani angeingia humo, ila akaona kama vipi, acha asubiri.

Jigga alikuwa bize ndani, alisubiri na kusubiri, kama masaa manne hivi, Jigga akatoka, walinzi walimzunguka, huku dogo akiwa hajui hili wale lile, akaanza kumfuata Jigga. Unamfikiaje sasa? Baunsa wakaanza kumpa kipondo mpka Jigga alipowaambia waache kwani haikuwa fea kumpiga mtu bila kosa.

Akamuuliza alitaka nini? Dogo akatoa cd na kumpa, akamwambia alikuwa na ndoto za kuwa mwanamuziki mkubwa, hakujua atakapoanzia, anaomba akasikilize hiyo cd, Jigga hakuwa na shida, akachukua na kusepa huku akiwa na ile cd iliyokuwa na contact za dogo.

Dogo akasikilizia simu, kimyaaaa, dogo kila akilala na kuamka, alikuwa anaangalia simu, kilanamba ngeni alipiga lakini haikuwaya Jigga, moyoni akaumia sana.

Baada ya miaka kadhaa, Jigga akapata wazo la kufungua lebo yake ya Roc Nation, akaanza kuwafikiri wasanii ambao wangetakiwa kuwa humo, kwenye kufikiria huko si ndiyo akamkumbuka dogo?Akaichukua ile cd na kuanza kuisikiliza.

Oyaaa! Jigga akajuta kwa nini hakuisikiliza tangu mika aile aliyopewa na dogo. Beat zilikuwa kali na dogo alikamua kupita kawaida. Akaamua kumpigia.

Baada ya miaka mingi, huku akiwa amekata tamaa, dogo anasikia simu inaita, namba ngeni, hakuhisi kabisa kama ingekuwa ya Jigga kwani alishasahau na kuendelea na mitikasi yake, akaipokea na kuipeleka sikioni.

Aliyemsikia ni mpambe ambaye alimwambia Jigga alitaka kumuona. Dogo hajaoga, akaondoka kuelekea alipoelekezwa.

Kufika huko akakutana na Jigga mwenyewe, akaanza kuzungumza naye, alimuuliza hizi beat katengeneza nani? Dogo akajibu yeye mwenyewe. Jigga akaona huyu dogo mkali, akamuingiza kwenye Roc Nation.

Unamjua dogo mwenyewe?

Kwa jina anaitwa Joe Cole.
 
Nadhani mimi enzi hizo nilikuwa na kipaji cha boli! ,ila kukosa usimamizi na changamoto ya kutafuta ugali....udambwi umepotea...ningekuwa Epl au Paris napiga minoti.
 
Back
Top Bottom