ngara23
JF-Expert Member
- Aug 31, 2019
- 9,091
- 21,087
Watu wengi wanafirisika biashara Kwa kufuata mkumbo wa kufungua maduka, bar, vibanda n.k
Yaani mtu una million 2 au 3 unachukua mzigo wa kuweka dukani?
Ndugu utalia sana aisee,
Vijana wanatoka vyuo wanapewa mtaji na wazazi wanakimbilia kufungua boutiques, sijui bar, n.k na mtaji umepewa million3 tutaishia kulia na kulipa Kodi TRA, jiji, frem, walinzi n.k
Tafuta mteja Kwa bidii ndo umletee bidhaa anayohitaji
Au ndo umepata sijui laki 4 unakimbilia kufua biashara ya matunda yatakuozea utalia sana.
Biashara na wateja wa siku hizi sio wa kwenda madukani, sijui sokoni au mgahawani kula Kwa mama ntilie watu wanapenda wapelekewe huduma hapo walipo
Kwa mfano kama unauza chakula pita sehemu watangazie au mitandao tangaza pata oda pika chakula kutokana na wateja wa siku hiyo, na siyo upike kg 50 za Michele hujui atakula nani, tutaishia kumwaga tu mavyakula yako
Kama unauza mavazi tafuta njia ya kutafuta watu wa kukuagiza niletee nguo A B C ndo uende kariakoo uchukue mzigo unaohitajika Kwa wateja, utauza na mzigo unakwisha na faida unaiona,
Sio unaamka unalangua manguo ambayo hatujui atayanunua nani, utapigwa dolo upauke
Jitahidi kutangaza biashara na kuchukua oda ya mzigo kabla ya kulangua ili kulinda mtaji usifirisike
Kwa wenye mitaji mikubwa kama millions 50 hao sawa kuagiza mzigo hata kama hana oda ni rahisi kubali sokoni na kupambana maana ana mabavu ya kutosha.