Mkuu, ikiwa wazazi wako walikupeleka shule na leo upo mtaani eti unalalamika kwamba hauna mtaji, basi jiweke kwenye kundi la vijana waliowatia hasara wazazi wao.
Naomba nijibu hoja zako kama ifuatavyo:-
1. Kukosa mtaji ni uzembe mkubwa na kimsingi hakuna mtu ambaye anaweza kupata mtaji kwa urahisi kama mnavyo dhania ndugu (nendeni mkabebe haya zege ama kuchimba mitaro ili mtaji upatikane)
2. Hakuna mtu mwenye anapenda kufanya kazi ngumu, na hasa vijana wengi wa kiTanzania ni wavivu wa kupindikua (vijana wa leo hawapendi kazi za mikono na wana madeko sana)
3. Sio wote wanao fanikiwa walipata ujuzi wa kazi za mikono. Na kukosa nafasi ya kujiunga ama kuchagukiwa chuo kikuu, hiyo haimaanishi kwamba basi ushindwe kuuza hata matunda mitaani ama kubrashi hata viatu.
4. Hakuna connection ambayo utaweza kuipata kama hauna mwenye atakushika mkono(hii isiwe kigezo kwa vijana na hasa ndipo hasa mnapaswa muanze kujipanga mapemza ikiwa unajua kwamba hauna connection).
5. Stress sio kitu kinacho kuja ghafla ndugu, kila jambo linahitaji utulivu na umakini ili kujikinga na mikwamo isiyo ya lazima kama kuwapa stress na desperation.