Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
UKIWA UMEKATA TAMAA, CHUKUA HII.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Bila kukupotezea muda.
1. Unaweza kukosa Elimu lakini huwezi kukosa Akili. Zingatia Akili ndio itakayokusaidia kuishi Maisha unayotaka.
2. Unaweza kukosa Dini lakini huwezi kukosa Imani. Elewa kuwa hauhitaji dini kumjua na kuona Matendo ya Mungu Ila unahitaji Imani kumjua na kuona Matendo ya Mungu.
Elewa kuwa Dini haikufanyi uwe na tumaini, ujasiri na uthubutu katika Maisha. Ila Imani ndio inakupa Tumaini, ujasiri na uthubutu katika Maisha.
Chochote utakachokifanya kwenye Maisha kitaamuliwa na Akili kisha Imani. Na sio Elimu wala Dini.
Akili yako itakuambia ufanye Jambo Fulani, hiyo ni kazi ya Akili (fikara, wazo, mtazamo, n.k). Imani ndio itakupa Tumaini, ujasiri na uthubutu wa kulifanya Jambo Hilo. Kisha Akili itakupa mbinu(maarifa) na mikakati ya kutekeleza Jambo Hilo.
3. Unaweza kukosa ndoa lakini huwezi kukosa Mapenzi.
Watu huhangaikia Kupata ndoa lakini kamwe Watu hawawezi kuhangaikia Kupata Mapenzi. Kwa sababu mapenzi yapo ndani ya MTU. Huwezi kuhangaika kutafuta Jambo ambalo lipo ndani ya nafasi yako.
Wengi hushindwa kutofautisha Mapenzi na Ndoa.
Wengi hutafuta mapenzi ya Watu wengine(ndoa) badala ya mapenzi ya hao Watu wengine na Yao yanatakiwa yatafutane.
4. Unaweza kukosa nyumba(house) lakini huwezi kukosa Makazi(home).
Nyumba ni Kitu au jengo lakini Makazi(home) ni mahali panapokupa furaha na Amani.
Nyumba haikupi Amani Kwa sababu Amani Ipo ndani yako. Na Amani haitoki nje ya mwili wako Bali ndani ya moyo wako.
Kwa leo tuishie hapa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam