Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 620
- 1,240
Kampuni ya apple imesema itatoa Zawadi ya dola milioni moja kwa yeyote atakayeweza kudukua mfumo wao mpya wa seva za akili bandia (AI) kwenye apple intelligence.
Kampuni hiyo iliweza kutangaza hiyo taarifa siku ya Alhamisi kwa kusema kwamba "inawaalika wadau au wataalamu mbalimbali wenye Uwezo wa kudukua taarifa kuweza kudukua seva Yao kwa kufanya majaribio kujua udhaifu wa mfumo wao huko wapi".
Kwani kampuni hiyo imetangaza kuachia apple intelligence wiki ijayo wakati iOS yao ya 18 itazinduliwa jumatatu ya tarehe 28.
Apple intelligence itaweza kupatikana kwa watumiaji wa iphone , ipad, macs ndani yake kutakua na tools mbalimbali zitakazo kusaidia kwenye kuandika, clean up, notification , Siri nk.
Ulipwaju unaweza kuwa mkubwa kwa mtu ambaye atakayeweza kuingia kwenye mfumo na kuweza kuhalibu mifumo mbalimbali na kutotambulika.
#bongotech255 #Apple #applehack #Udukuzi #Fahamu #AppleTanzania