May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Kwa sasa sio ajabu kumsikia Shabiki anamtolea maneno yasiyo na staha Mchezaji kwa vile tu hajaridhishwa na alivyocheza mechi kadhaa zilizopita wakakosa matokeo chanya.
Kwa mfano Mtu atasahau kabisa kuwa Boko ndiye alichangia zaidi ya nusu ya magoli yaliyopelekea timu yao kuwa Mabingwa wa nchi na hata kung'ara kimataifa.
Mpira ni Magoli, na kama mnakuwa na Mchezaji anayeweza kufunga muda wowote na amewahi kudhihirisha hivyo kwa msimu uliopita ni kwa vipi tena kukosa subira kwake?
Kwa sasa Simba wanamfurahia Ajib, si vibaya na hongera kwake kwa kuzikonga nyoyo ya Mashabiki kwenye mechi iliyopita, lakini tusimvimbishe kichwa akapotea au kumpa mzigo wa presha akashindwa kuhimili na vile vile tusiwasahau wenzake waliopo kwenye timu, maana timu ni timu, yaani timu ni Wachezaji wote 11.
Usimtukane Mchezaji mmoja ukamsifia sana mmoja tukasahau wao wote ndio wanaounda timu.