Uchaguzi 2020 Ukiwasikiliza kwa makini sana Tundu Lissu na Askofu Gwajima utaona dalili zote za mwisho wa Ulimwengu huu

Uchaguzi 2020 Ukiwasikiliza kwa makini sana Tundu Lissu na Askofu Gwajima utaona dalili zote za mwisho wa Ulimwengu huu

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Katika Biblia takatifu nabii wa uongo anatafsiriwa kama mtu ajifanyaye Nabii ama kwa kujidanganya au kudanganya.

Nabii wa uongo ni yule aelezaye maono yenye hila na ulaghai ambayo kamwe hayawezi kukamilishwa.

Tundu Lissu anazungumzia kutoa Bima ya afya kwa watu wote nchini raia na wasio raia, hii ni ahadi yenye hila.

Askofu Gwajima anaahidi kuwapeleka Marekani wananchi wote wa jimbo la Kawe huu ni unabii wa uongo.

Hivi Watanzania, hatuwezi kufanya siasa zilizosheheni ukweli?

Maendeleo tuliyoyapata kwa miaka 5 tunayaona kwa macho yetu tusikubali kudanganywa na vibaraka wa mabeberu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kuna watu kwenye siasa hawapewi nafasi za kugombea kwasababu wao wanazimudu bali kwaajili ya purpose ya wengi kwenye itakidi ya wenye uelekeo mmoja.
 
Kuna watu kwenye siasa hawapewi nafasi za kugombea kwasababu wao wanazimudu bali kwaajili ya purpose ya wengi kwenye itakidi ya wenye uelekeo mmoja.
 
Ni mipango tu, yeye kaamua kujenga madaraja na kuacha watanzania wakidhoofu kwa njaa na matibabu hafifu.
 
Katika Biblia takatifu nabii wa uongo anatafsiriwa kama mtu ajifanyaye Nabii ama kwa kujidanganya au kudanganya.

Nabii wa uongo ni yule aelezaye maono yenye hila na ulaghai ambayo kamwe hayawezi kukamilishwa..
Mbona sera ya Bima kwa wote CCM mna sema ni yenu??? Au tukampige mawe Dr kitila?
 
Katika Biblia takatifu nabii wa uongo anatafsiriwa kama mtu ajifanyaye Nabii ama kwa kujidanganya au kudanganya.

Nabii wa uongo ni yule aelezaye maono yenye hila na ulaghai ambayo kamwe hayawezi kukamilishwa...
50M Kila kijiji ilikuwa unabii mkubwa wa uongo!!
 
Kamwe Tundu Lissu huwezi kumuweka kapu moja na Gwaji boy.
never on earth!
Gwajiboy yeye ajikite kula za waumini wake!! Mzee wa kufufua mizuka na misukule huko huko...Kawe hii itakwenda kumwadhibu vibaya mno... na kanisa lake kishaligawa ki itikadi...sadaka ishaporomoka.
 
bado tunakazi kubwa ya kuibadilisha Tanzania baadhi ya wanasiasa wenyewe hawajielewi na wananchi ndio kabisa tumejifia na kujiozea tunaongozwa na mihemko tu na siyo tafakuru nzur dah tutaongozwa vibaya adi mwisho wa dunia
 
Wewe ni Ibilisi na unawaza ya kiibilisi tu. Hayo ya Gwajima yanaweza yasiwezekane lakini mengine yawezekana kwa jina la Mola! Amina!
 
Katika Biblia takatifu nabii wa uongo anatafsiriwa kama mtu ajifanyaye Nabii ama kwa kujidanganya au kudanganya.

Nabii wa uongo ni yule aelezaye maono yenye hila na ulaghai ambayo kamwe hayawezi kukamilishwa....
Uzuri Biblia ilitufunulia njia ya kuwatambua hawa manabii wa uongo. "Mtawatambua kwa matunda yao". Kama anaahidi demokrasia, jiridhishe kwamba ni mtu wa demokrasia kwa kutazama huko anakotoka.
 
Uzuri Biblia ilitufunulia njia ya kuwatambua hawa manabii wa uongo. "Mtawatambua kwa matunda yao". Kama anaahidi demokrasia, jiridhishe kwamba ni mtu wa demokrasia kwa kutazama huko anakotoka.
Hakika mkuu!
 
Unafanya kosa kubwa sana Kumuweka Mwamba Lisu kwenye kapu moja na Gwajima.
Tuombe radhi
 
... mlisema elimu bure haiwezekani na mara baada ya uchaguzi wa 2015 imekuwa mojawapo ya mambo yanayopigiwa chapuo kuwa yametekelezwa na CCM!
 
Back
Top Bottom