Ndugu yangu usiongee kwa mihemuko, jaribu kuelewa mada
ninachokisema ni kwamba baba tale na salamu sisemi wao ndiyo wawe wasemaji bali babu tale na salam wao nimewatumia kukuonyesha kazi wanayoifanya kwa diamond platinum. wamemfikisha wapi?
wasanii wanahitaji watendaji wa kunyanyua sanaa yao kutoka ilipo sasa ambapo ni kama hatua aliyokuwepo diamond platinum miaka hiyo. Leo wamemfikisha wapi ndiko watu wanaotakiwa kutumiwa na wasanii watazame tasnia ya muziki yote ipande hivyo.
Sasa steve ni mtu wa aina kama ya haji manara, wao ni wahamasishaji, kutangaza jina. Mtu wa kusema maneno mengi. hawa ni watu wanaofaa kwenye vilabu vya mpira kuhamasisha mashabiki, kwenye makampuni kuhamasisha wateja lakini umoja wa wasanihii unahitaji watu wa mipango itakayokuja kunufaisha industry kwa pamoja.
ukiwasikiliza wasanii kwa makini utaelewa wapo wenye upeo wanaojua kazi za umoja sio kuhamasisha kutangaza jina la umoja lakini wawe watu ambao wanaweza kuchungulia sheria zina mapungufu gani wakapendekeza, wawe ni watu wanaoweza kuangalia huko nje kinafanyika nini kwa wasanii kilichwaendeleza wakajaribu kukopi, wawe ni watu wanaoweza kutazama fursa za kibiashara kama uingiaji mikataba mbalimbali wakashauri.
shida nyinyi mnatazama mtu wa kupiga kelele kwenye vyombo vya habari na hiyo kazi steve anaiweza lakini wao wanaona hawatafuti mtu wa kufanya hivyo bali mtu wa kuwa mtendaji kufanya wasiyoyaweza wao