Ukiwezeshwa na kupewa jukwaa la kusemea, je ungetetea au kupinga nini na kwanini?

Ukiwezeshwa na kupewa jukwaa la kusemea, je ungetetea au kupinga nini na kwanini?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Mimi ningepinga uharibifu wa mazingira unaofanywa kwa kisingizio cha maendeleo. Ninakerwa mno na ukataji wa miti ovyo ili kujenga barabara au miradi kama ule wa bwawa la Nyerere.

Ningekemea mno uharibifu wowote wa mazingira bila kujali sababu gani imefanya hivyo. Yaani hata miradi yote inayosababisha uharibifu wa mazingira ningepinga.

Wewe ungefanya nini?
 
Kiukweli mi ningesema juu ya wanachotufanyia nymba za kulala wageni

Mimi ni fundi kazi yangu kuna muda inanilazimu kutoka mkoa niliopo(dar) na kwenda kufanya kazi katika mikoa mengine iwe ya jirani au ya mbali zaidi. Kero yangu tunapofika nyumba za kulala wageni. Chaajabu au kinachonishangaza na kunikera mtoa vyumba haruhusu kulala chumba kimoja jinsia moja yaani wanaume wawili. Tena wanakataa sirias kabisa ukihoji wanakujibu polisi huwa wanakuja usiku kuwagongea na kutaka kujua mmelala vipi kama mpo jinsia moja watu zaidi ya mmoja chumbani mizozo inaanzia hapo kwamba mnapelekwa kituoni kwa sababu ya kuwa mnahamasisha ushoga. Dah ukiangalia maskini ya mungu usikute kanauli kenyewe mnakopa mnajinyima na kubana matumizi halafu unakuta mdada wa gesti anakuja na kauli za kishujaa kama hizo. Sasa sijui ni sababu za kibiashara kwamba ili kilamtu alale chumba chake vyumba vijae au maana yao nini

Mana mtu akitaka kufanya huo ushoga wake atafanyatu.
 
Mi ntasema tunajikosesha maendeleo wenyewe kwa kutumia maneno yasiyo sahihi.

Mfano badala tuseme nchi yetu inapambana na UMASKINI, UJINGA NA MARADHI..... tutumie kwamba nchi yetu inapambania UTAJIRI, AFYA NA AKILI.

Maana ona mfano kama hata wewe mtoa mada ungekuwa umejiwekeza zaidi kwenye kuboresha na kuhifadhi mazingira. Kwa kiasi fulani ungeuona huo ujenzi wa bwawa la maji kama kuokoa mazingira;
Kuongeza matumizi ya umeme katika usafirishaji SGR na electric cars and bikes
Kuongeza matumizi ya hydroelectic power kwenye upishi itaokoa misitu
Kuongeza matumizi ya umeme........

Anyway umeelewa.

Kingine ni salamu. Hii shkamoo ipigwe marufuku. Inakiharibu kizazi kijacho kabla hata hakijawa na akili. Shkamoo inazalisha sana ma chawa na watu wenye kung'angania adabu badala ya heshima
 
Kiukweli mi ningesema juu ya wanachotufanyia nymba za kulala wageni

Mimi ni fundi kazi yangu kuna muda inanilazimu kutoka mkoa niliopo(dar) na kwenda kufanya kazi katika mikoa mengine iwe ya jirani au ya mbali zaidi. Kero yangu tunapofika nyumba za kulala wageni. Chaajabu au kinachonishangaza na kunikera mtoa vyumba haruhusu kulala chumba kimoja jinsia moja yaani wanaume wawili. Tena wanakataa sirias kabisa ukihoji wanakujibu polisi huwa wanakuja usiku kuwagongea na kutaka kujua mmelala vipi kama mpo jinsia moja watu zaidi ya mmoja chumbani mizozo inaanzia hapo kwamba mnapelekwa kituoni kwa sababu ya kuwa mnahamasisha ushoga. Dah ukiangalia maskini ya mungu usikute kanauli kenyewe mnakopa mnajinyima na kubana matumizi halafu unakuta mdada wa gesti anakuja na kauli za kishujaa kama hizo. Sasa sijui ni sababu za kibiashara kwamba ili kilamtu alale chumba chake vyumba vijae au maana yao nini

Mana mtu akitaka kufanya huo ushoga wake atafanyatu.
Umenigusa sana jamaa yangu....hawajui tu namna tunavyojibana hata kula. Kila siku ugali dagaa ugenini ili mgongee sehemu ya kulala japo mwisho wa kazi urudi na kafungu kwa ajili ya familia....
 
Back
Top Bottom