Kiukweli mi ningesema juu ya wanachotufanyia nymba za kulala wageni
Mimi ni fundi kazi yangu kuna muda inanilazimu kutoka mkoa niliopo(dar) na kwenda kufanya kazi katika mikoa mengine iwe ya jirani au ya mbali zaidi. Kero yangu tunapofika nyumba za kulala wageni. Chaajabu au kinachonishangaza na kunikera mtoa vyumba haruhusu kulala chumba kimoja jinsia moja yaani wanaume wawili. Tena wanakataa sirias kabisa ukihoji wanakujibu polisi huwa wanakuja usiku kuwagongea na kutaka kujua mmelala vipi kama mpo jinsia moja watu zaidi ya mmoja chumbani mizozo inaanzia hapo kwamba mnapelekwa kituoni kwa sababu ya kuwa mnahamasisha ushoga. Dah ukiangalia maskini ya mungu usikute kanauli kenyewe mnakopa mnajinyima na kubana matumizi halafu unakuta mdada wa gesti anakuja na kauli za kishujaa kama hizo. Sasa sijui ni sababu za kibiashara kwamba ili kilamtu alale chumba chake vyumba vijae au maana yao nini
Mana mtu akitaka kufanya huo ushoga wake atafanyatu.