GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Joseph Kasheku Msukuma na Jumanne Kishimba "hawajashule" kiviile, lakini si wajinga. Ni miongoni mwa wanasiasa wanaoongoza kwa kuwabeza wasomi wa Kitanzania.
Kuna baadhi ya watu wameonesha kukasirishwa na kejeli za hao wanasiasa, lakini ukifuatilia kwa makini, utabaini mengi ya madai yao yana mashiko.
Hata msomi makini, CAG mstaafu, Profesa Musa Assad, alishawahi kusema kuwa asilimia sitini ya watumishi wa Serikali hawana uwezo. Serikali ililipinga hilo vikali, lakini madudu ya watumishi wake yameendelea kuiumbua.
Nimeliona sekeseke linaloendeshwa na Makonda mkoani Arusha. Watumishi wengi wanaonekana wanapwaya sana kwenye nafasi zao. Naweza kusema "hawajielewi"
Lakini kwa nini iwe hivyo? Hayo yameanzia mbali. Ni tokea wakiwa vyuoni. Wengi hawakuwa "serious" na masomo, bali kulitumbua bumu walilopewa na Serikali. Labda wa siku hizi wako makini, pengine.
Kipindi nikiwa Chuoni, nilishuhudia jinsi wengi wa wanavyuo walivyokuwa wakiendekeza maisha ya anasa. Kidogo waliokuwa wakijitahidi ni wa shahada za udaktari, ualimu, "Engineering", n.k. Lakini wengi wa waliosalia, hasa wa vitivo vya Sanaa, walikuwa ni watu wa starehe sana (japo si wote).
Weekend ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu ili waende kwenye kumbi za starehe. Kesho yake utasikia wengine wakijisifia kuwa siku iliyopita walikuwa club moja na Mbunge fulani n.k.
Sasa kama hao ndio wasomi wenyewe, wanatarajiwa kuwa na lipi jipya wakati hawakujiandaa ipasavyo kwa majukumu hayo?
Kishimba aliposema kuwa asilimia tisini ya wasomi wa Tanzania wanajua tu kusoma na kuandika hakukosea.
Wasomi nchi hii ni wachache sana kuliko takwimu zinavyoonesha. Wengi wa walio na vyeti si wasomi ilhali kuna wasomi wasiokuwa na vyeti.
Miongoni mwa hao watu ambao ni wasomi japo hawana vyeti ni Jumanne Kishimba.
Sijui kwanini hawampi "uprofesa" wa heshima😀