Ukiyafahamu maisha ya wanavyuo kwenye vyuo vya Elimu ya Juu nchini, hutawalaumu wanaowabeza wasomi wa Kitanzania

Ukiyafahamu maisha ya wanavyuo kwenye vyuo vya Elimu ya Juu nchini, hutawalaumu wanaowabeza wasomi wa Kitanzania

Joseph Kasheku Msukuma na Jumanne Kishimba "hawajashule" kiviile, lakini si wajinga. Ni miongoni mwa wanasiasa wanaoongoza kwa kuwabeza wasomi wa Kitanzania.

Kuna baadhi ya watu wameonesha kukasirishwa na kejeli za hao wanasiasa, lakini ukifuatilia kwa makini, utabaini mengi ya madai yao yana mashiko.

Hata msomi makini, CAG mstaafu, Profesa Juma Assad, alishawahi kusema kuwa asilimia sitini ya watumishi wa Serikali hawana uwezo. Serikali ililipinga hilo vikali, lakini madudu ya watumishi wake yameendelea kuiumbua.

Nimeliona sekeseke linaloendeshwa na Makonda mkoani Arusha. Watumishi wengi wanaonekana wanapwaya sana kwenye nafasi zao. Naweza kusema "hawajielewi"

Lakini kwa nini iwe hivyo? Hayo yameanzia mbali. Ni tokea wakiwa vyuoni. Wengi hawakuwa "serious" na masomo, bali kulitumbua bumu walilopewa na Serikali. Labda wa siku hizi wako makini, pengine.

Kipindi nikiwa Chuoni, nilishuhudia jinsi wengi wa wanavyuo walivyokuwa wakiendekeza maisha ya anasa. Kidogo waliokuwa wakijitahidi ni wa shahada za udaktari, ualimu, "Engineering", n.k. Lakini wengi wa waliosalia, hasa wa vitivo vya Sanaa, walikuwa ni watu wa starehe sana (japo si wote).

Weekend ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu ili waende kwenye kumbi za starehe. Kesho yake utasikia wengine wakijisifia kuwa siku iliyopita walikuwa club moja na Mbunge fulani n.k.

Sasa kama hao ndio wasomi wenyewe, wanatarajiwa kuwa na lipi jipya wakati hawakujiandaa ipasavyo kwa majukumu hayo?

Kishimba aliposema kuwa asilimia tisini ya wasomi wa Tanzania wanajua tu kusoma na kuandika hakukosea.

Wasomi nchi hii ni wachache sana kuliko takwimu zinavyoonesha. Wengi wa walio na vyeti si wasomi ilhali kuna wasomi wasiokuwa na vyeti.

Miongoni mwa hao watu ambao ni wasomi japo hawana vyeti ni Jumanne Kishimba.

Sijui kwanini hawampi "uprofesa" wa heshima😀
We jamaa bana... Mwambie huyo ndugu yako atuwekee lami kwanza hapa Kahama
 
Inawezekana amekuwa akifanya hivyo!

Kwani alichoshauri kina ubaya wowote? Mbona ni wazo zuri?
Yale yale kuna MSHENZI alipewagwa uwaziri akataka afute Masomo ya sayansi aache Masomo ya Biashara alafu kwa ushenzi akaunganisha Commerce n Book Keeping pamoja kujitia yeye anajua sana Biashara walipokuja wengine wakamtoa kwenye reli Masomo ya sayansi yakarudishwa

Sasa mtu km huyu akipewa uwaziri wa Elimu atatuletea vituko kwenye mitaala yetu ya Elimu atatuletea Mada za kuuza Duka la Spea za Magari na Maduka ya Chakula eti Somo la kutafuta Hela kwanini wanafunzi wanaambiwa ukiwa umesoma na kwenu kuna nyumba na Mifugo uza Mifugo ufanye mtaji kujiendeleza kielimu HIO pia kaichambua kwenye kitabu na kuitolea macho anataka watoto wafundishe Jinsi ya kuuza Askrimu za Bakhresa na Juice za Ukwaju, yaan Somo la kutafuta Pesa however he may be right on one side but not right on the other side
 
We jamaa bana... Mwambie huyo ndugu yako atuwekee lami kwanza hapa Kahama
Ni majuzi tu ndiyo nilianza kuzisikiliza clips zake. Sifahamiani naye mkuu, ila nimeona vitega uchumi vyake kadhaa Katoro mkoani Geita. Ana utitiri wa majengo.

Hata majengo ya CCM Katoro nasikia ameingia ubia na Chama chake ayakarabati halafu ayapangishe mpaka hela zake zirudi.
 
Nini CHANZO Cha utajiri wake Mkuu?
 
Kwahiyo mtu asile bata?
Nadhani hata mimi sikatai mtu kusoma na kula bata ila tu kuna mengi mno vyuoni hivi hujawahi ona kuna watu wanafanyiwa assignments, wanapewa marks na ma lecturer na mengine mengi.

Mbona nchi za wenzetu humu humu afrika wanafanya starehe ila elimu zao wanaweka mikazo sisi ni kama hatuna u serious kabisa.
 
Na siku ukihitaji kufanyiwa operesheni ya moyo waite hao akina Kishimba wako na Musukuma waje wakufanyie!

Hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na mfumo imara wa elimu. Tuboreshe mfumo wetu wa elimu ili wasomi wetu angalau waweze kuendana na kasi ya dunia HASA katika maeneo ya STEM (Science, Technology, Engineering and Math); na kufikia kiwango cha kuajirika duniani kote.

Kubeza na kutukana wasomi utafikiri wasomi hao wanaishi katika ombwe ni ujinga; na hili linaakisi jamii ya kijinga (siyo ya kipumbavu) tuliyonayo!

Ati, utamlaumuje samaki aliyejikuta amefugwa katika kizimba kichafu kinachonukia uchafu na harara? Na mwenye kizimba (wanasiasa) ndiyo kwanza wanazidi kuongezea uchafu na hata sumu (isiyoua) kizimbani?

Pengine ndiyo maana Kishimba watoto wake wote kasomeshea nje! Anajua umuhimu wa elimu BORA!
 
Ati, utamlaumuje samaki aliyejikuta amefugwa katika kizimba kichafu kinachonukia uchafu na harara? Na mwenye kizimba (wanasiasa) ndiyo kwanza wanazidi kuongezea uchafu na hata sumu (isiyoua) kizimbani!

Pengine ndiyo maana Kishimba watoto wake wote kasomeshea nje! Anajua umuhimu wa elimu BORA!
Kwani Kishimba kasema ni daktari wa tiba za binadamu?

Si Kishimba peke yake ndiye aliyeona mapungufu ya wasomi wa Tanzania. Hata msomi nguli, Profesa **** Assad alishawahi kulibainisha hilo. Alisema kuwa asilimia sitini ya watumishi wa uma uwezo wao
ni mdogo katika kutimiza majukumu yao ya kikazi.

Siyo kwamba nchi haina wasomi kabisa, wapo, lakini wengi wa "the so called" wasomi ni watupu "upstairs".

Wewe unafikiri ni kwa nini akina Zitto, Tundu Lissu, na Dr. Slaa walikuwa wakiichachafya Serikali bungeni enzi zao? Ni kwa sababu ni "wasomi".
 
Siojaona shida ya kuendekeza club na kushindwa kuwa smart au kutoweza kufanya kazi ya mtu.
 
Na siku ukihitaji kufanyiwa operesheni ya moyo waite hao akina Kishimba wako na Musukuma waje wakufanyie!

Hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na mfumo imara wa elimu. Tuboreshe mfumo wetu wa elimu ili wasomi wetu angalau waweze kuendana na kasi ya dunia HASA katika maeneo ya STEM (Science, Technology, Engineering and Math); na kufikia kiwango cha kuajirika duniani kote.

Kubeza na kutukana wasomi utafikiri wasomi hao wanaishi katika ombwe ni ujinga; na hili linaakisi jamii ya kijinga (siyo ya kipumbavu) tuliyonayo!

Ati, utamlaumuje samaki aliyejikuta amefugwa katika kizimba kichafu kinachonukia uchafu na harara? Na mwenye kizimba (wanasiasa) ndiyo kwanza wanazidi kuongezea uchafu na hata sumu (isiyoua) kizimbani?

Pengine ndiyo maana Kishimba watoto wake wote kasomeshea nje! Anajua umuhimu wa elimu BORA!
20231224_095052.jpg
 
Kwanza tukubaliane sehemu kubwa Ujinga unaanzia shule na tueleze ujinga kama upungufu wa maarifa..
Sasa mfano wa hawa watu wawili..10 or more yrz back then students assignment au kazi yoyote ya shule ilikuwa ikitolewa ni lazima utasoma kitabu physical au hata kama ni online utapitia articles kisha utaandaa summary na kuandika kile ulichojifunza.
Kazi uliyokuwa unasoma library na kufanya siku kadhaa kuandaa paper sasa hivi mwanafunzi swali anaplug kwenye ChatGPT tena kwenye simu kazi inafanyika ndani ya dk 1, anacopy nakupaste kazi ambayo hata hajui humo ndani imeandikwa kitu gani ila anapata marks 10 over 10 ila kichwani mweupe hana maarifa yoyote.
Hatari nayoizungumzia ndiyo hiyo wasomi wengi wakitanzania sijui itakuaje mana ni weupe,
ChatGPT inatoa majibu in general view siyo in deep, kama Mwalimu anatoa 10/10 kwa majibu yaliyotolewa na chatGPT basi huyo mwalimu bila shaka typo shallow.
 
Back
Top Bottom