Ukizingatia haya hautapata shida kuongea na mwanamke

Ukizingatia haya hautapata shida kuongea na mwanamke

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Usipate shida kuhusu uongee nini na mwanamke, sababu wanawake wanajali unavowafanya wajisikie ukiwa nao zaidi ya maneno unayoongea. Kadri unavyojiamini ndivyo mwanamke anakuamini pia. Hivyo cha muhimu kufanyia kazi ni kuboresha hali yako ya ujasiri wa kiume na kuzingatia haya wakati unaongea na mwanamke, haijalishi ni mara ya kwanza kuongea nae au ni mke wako wa miaka 40.

ngalie machoni. Kwa mimi nimeona mara nyingi kadri ninavyowaangalia wanawake machoni ndivyo wanavyolegea na kufunguka zaidi. Macho ni mlango wa roho. Hivyo jitahidi umuangalie machoni, na mkiangaliana ni jambo jema zaidi. Kuna tabia ya kuongea huku tunachezea simu, achana nayo mara moja, na anza kuangalia watu machoni unapoongea nao.

Ongea sauti ya kumfanya ajisikie amani. Usikakamae au kuwa siriaz sana, ongea taratibu kwa sauti kama unachombeza/ kubembeleza ivi ila kwa ujasiri na kujiamini. Hii itamfanya ajisikie amani na kupunguza kujilinda. Wewe mwenyewe jiachie.

Usichuje maneno yako. Wanawake ni watu wa hisia sana, hivyo chochote utakachoongea cha kumfanya ajisikie kitu ujue unafanya vizuri. Unakumbuka wakati tupo shule, wale waliokua wanaongea wanavojisikia wanawake ndo waliwapenda, ila wale waliokua wanaongea kwa kujibanabana ili asimuumize mtu ndio waliishia kuwanunulia wanawake sambusa tu. Unapoongea vile unavyojisikia kwa mwanamke anaona we ni mkweli mana mara nyingi mwanamke anajua unavyojisikia hata kabla hujaongea.

Pia usipochuja mawazo yako hautokosa cha kuongea na mwanamke. Lakini simaanishi kuongea maneno ambayo yanawafanya wanawake kujilinda/ kukukataa, mfano kujisifia sana au kumsifia sana au kumtukana.

Ongea taratibu kwa kujiamini. Kuongea taratibu kunamfanya mtu yoyote unayeongea naye akusikilize. Mwanamke ataweka hisia zake zaidi kutaka kujua nini utaongea hivyo atakusikiliza kwa umakini.
Faida nyingine ya kuongea taratibu ni kwamba unakua unajua nini unaongea, hivyo utaweza kuchagua maneno ambayo yatamvutia zaidi mwanamke wako kabla hujayasema.
Pia usisahau kumchombeza na kumfanya acheke/ afurahi.

Usipelekeshwe na hisia. Mwanamke atajaribu kukuyumbisha ili kuona je ni kweli unajiamini au unaigiza tu. Hivyo kuwa makini usiwe wa hisia sana kama mwanamke. Ukishaweka lengo usiyumbishwe.

Zingatia hayo unapoongea na mwanamke yeyote, awe mama yako, rafiki yako, boss wako wa kike au mke wako. Sababu utafanya mazungumzo kuwa mepesi na mwanamke atakuamini zaidi kukuambia vitu vingi. Wengi wanaolalamika wanawake ni wabaya/ hawaeleweki ni kwamba hawajui jinsi ya kumfanya mwanamke ajiachie na aongee naye vizuri na kumuambia vitu kiundani zaidi
 
Usipate shida kuhusu uongee nini na mwanamke, sababu wanawake wanajali unavowafanya wajisikie ukiwa nao zaidi ya maneno unayoongea. Kadri unavyojiamini ndivyo mwanamke anakuamini pia. Hivyo cha muhimu kufanyia kazi ni kuboresha hali yako ya ujasiri wa kiume na kuzingatia haya wakati unaongea na mwanamke, haijalishi ni mara ya kwanza
Kwani mzee wangu kuna shida gan kuongea na mwanamke? Hizi nyuzi zenu kila siku mnaanzisha huku kuwahusu ndo maana wanavimba vichwa ...

Mnawapa nafasi kubwa ambayo hao wenyewe wanaona hawai fit , ifikie hatua hizi mada zipungue wazee. Na mkiendelea hivi kulia lia mtaendelea kupokonywa manhood yenu...
 
Mwanaume, Siku zote usimpotezee Muda Mwanamke. Nenda moja kwa moja kwenye Point.

Unataka ngono/Sex? Mwambie.
Unataka Mahusiano? Mwambie.
Unataka Urafiki? Usimwambie.

Huwezi kuwa na Urafiki na Mwanamke, ni either awe Mpenzi wako au Uache kumsumbua.

Be a Man, You deserve Better.
 
Back
Top Bottom