Ndg zangu wana JF,
Hivi mtu akiomba msaada wa ushauri ni busara kumtukana kwa kosa alilolifanya au unampa ushauri -uwe mzuri au mbaya?
Mimi nilichouliza wengi wamenijibu lakini nasikitika na pretenders!
I had a friend ambae mke wake alitaka kumkata shingo-kwa kisu kwa sababu ya ulevi na kurudi usiku, siku ya kumkata shingo bahati mbaya kumbe siku hiyo jamaa hakuwa amelewa sawa sawa, akamkata kidogo,lakini mume alipotoka hospitalini baada ya siku kama 14 za kulazwa akawaita ndg na marafiki wengi wa karibu na kuwaambia kinyume na wengi mnachotegemea nimewaita ili nimsamehe mke wangu-hivi ndio alivyojisikia na ilikuwa ni kinyume na ushauri wa wengi waliompa.
Sasa mimi katika njia yangu ya kuogopa kufa kwa ukimwi au kupunguza chances za kuogopa kufa kwa ukimwi,nimeamua kupunguza njia moja,sasa mtu ukiniuliza kwanini ulimfuata huyo mama wa 2, wakati ni jambo nimeishaliombea msamaha na nimekubali makosa unakuwa unataka niseme nini cha kukufurahisha.
Kama alivyosema mwana JF mmoja hapo juu, tuombeane,sio wote waliopata HIV kuwa walikuwa wajinga saaana!
Hii HIV does not depend on your brain only!mke wako anaweza kubakwa na mtu mwenye HIV asikwambie na ukakuta wote mmeambukizwa,wote tuna ndgu na watoto-si lazima jambo kama hili likukute wewe tu,sijui kama kuna mwanaume mwenye control kwa mke wake au vice versa,
Nawapenda nyote.
Tuombeane!