Uko tayari kumchagua tena huyo Mbunge wako 2025?

Uko tayari kumchagua tena huyo Mbunge wako 2025?

Aaaah haiwezekani ni bora nisipige, tena walivyo wanafiki nawaona sasa hivi wanajiweka karibu na wananchi kwa kuwa uchaguzi umekaribia.

wanagawa misaada, hela, wanasaidia vikundi vidogovidogo, mara wajenge madaraja na barabara za mchongo,mara waje vijiwe vya kahawa, sokoni.. eti kusikiliza kero zetu. Mambo makubwa ya jimbo wanashindwa kutetea kila kitu wakiwa bungeni ni NDIO NDIO NDIO

WANAFIKI WAKUBWA WAPITE HIVI, Muda mwingine naonaga bora kutokupiga kabisa maana upige usipige watashinda kwa njia wanazozijua wenyewe na kuleta maendeleo wakijisikia

Kibongobongo, kutegemea mbunge atakunufaisha binafsi ni kujidanganya
 
Mbunge ambaye hajagombana na viongozi wa halmashauri hadi mkoa huyo hajafanya kazi, hatakiwi kurudi bungeni.Tunaona Mhe Rais anavyogombana na watendaji mbalimbali, tunamuona Waziri mkuu anavyoita watu wajieleze, tume zinaundwa na matokeo tunayaona, lkn wabunge wetu wao kimyaa, hata diwani wanashindwa kumkemea.

Watumishi mbalimbali wanashindwa kuwakemea, sasa tukuchague tena ili utusaidie nini, au kwa vile hivi vibarabara 2,3 au visima vya maji vilivyokuja jimboni kingekewa ukizingatia lilikuwa ni ombi la miaka 20 iliyopita ndio mbunge atajidai navyo kuwa ameleta maendeleo.Ukiwapigia simu hawapokei, kisingizio eti kazi nyingi, sasa tukurudishe bungeni kwa lipi ulilofanya la maana.
 
Mbunge ambaye hajagombana na viongozi wa halmashauri hadi mkoa huyo hajafanya kazi, hatakiwi kurudi bungeni.Tunaona Mhe Rais anavyogombana na watendaji mbalimbali, tunamuona Waziri mkuu anavyoita watu wanieleze, tume zinaundwa na matokeo tunayaona, lkn wabinge wetu wao kimyaa hata diwani wanashindwa kumkemea, watumishi mbalimbali wanadhindwa kuwakemea, sasa tukuchague tena ili utusaidie nini, au kwa vile hivi vibarabara 2,3 au visima vya maji vilivyokuja jimboni kingekewa ukizingatia lilikuwa ni ombi lamiaka 20 iliyopita ndio mbunge atajidai navyo kuwa ameleta maendeleo.Ukiwapigia simu hawapokei, kisingizio eti kazi nyingi, sasa tukurudishe kwa lipi?
Mwambieni DAB awaambie na wabunge wapeleke report kwake,
 
Tanzanian huwa kuna uchaguzi huru? Wabunge waliopo karibia wote ni kwa hisani ya marehemu mwendazake,kupiga kura ni kujicholesha tu .
 
Salaam Wakuu,

Nina swali hapa

Endapo Mbunge wa Jimbo lako atagombea tena, utampigia kura za Ndiyo?

Kwanini?


Karibuni tufunguke
Naanzaje kumuacha Antony Mavunde kwa hapa Dodoma mjini kila kitu kinaletwa na serikali kuu bila hata yeye kukiomba. 2025 nitaenda naye hana baya na mtu hapa Dodoma mjini
 
Strength ya mwanasiasa hasa kwa nchi za Afrika haitokani na fedha alizonazo Bali kiwango cha ufahamu walio nao kwa wafuasi wake. Kwa maana hiyo wabunge wengi hasa ambao wanajua hawajafanya kitu kwenye majimbo Yao wanaamini watarudi vizuri tu kwasababu ya aina ya ufahamu wa watu wao.Kwa upande wangu nitatimiza jukumu langu la kupiga kura.
 
Siasa imekuwa na mambo ambayo kwa kiasi fulani yamekuwa hayaelezeki kwa urahisi.
Kuna kipindi ambacho wanasiasa huwa wanakuja na ahadi nyingi kwa wananchi wakati wa kampeni ila wanapopata nafasi hizo za uongozi kuna kuwa na daraja kubwa kati ya kiongozi na wananchi katika utekelezaji wa ahadi zilizotolewa .
 
Back
Top Bottom