Uko tayari kuwa mama wa kufikia/kambo?!


Sidhani,hebu soma post zingine hapo juu!
 
hii mada nashindwa hata kuchangia maana inanigusa kwa kiasi kikubwa

Pole sana,ndo maisha lakini.
Ujue kwenye mambo haya uwezo wa kiuchumi matters a lot.
Wanawake wengi wako radhi mtoto alelewe na baba na mama wa kambo ili mradi wapate elimu nzuri ambayo yeye anajua hawezi kuwapa akiamini wakikua na kufanikiwa watamsaidia uzeeni,which,to me,makes perfect sense.
 

Mh!Ni wanawake wachache sana wana mtazamo huu Bishanga!
 
OK. Lakini sidhani kama ni mtazamo mzuri kwani sidhani kama kuwa na mtoto/watoto kunawezasababisha uvunje mapenzi yako kwa umpendae!

I do agree with u,but nini kinasababisha haya?
 
Sidhani,hebu soma post zingine hapo juu!

Tatizo lako ni kwamba umeshajiandalia jibu la NDIO tu bila IFs na ndilo unalolitaka. Kama ungekuwa umewahi kuishi na watoto wa kambo ambao kila kukicha wanaona mama uao kaonewa ungejua kwanini sio rahisi tu kumbeba mtoto wa mtu kama kipisi cha puzzle na kukiFITisha kwenye puzzle ulo nayo. Mpaka wababa wenyewe hua wanaumwa vichwa, sembuse huyo mama anaeweza kuonekana jangili?
 
Mimi siko tayari kabisaaa labda kama mama wa mtoto amekufa akiwa hai no way abebe msalaba wake kwa raha zake.
 
Ishu ni kuwa tayari jamii imeathiliwa na mtazamo ya kuwa mama wa kambo ni mnyanyasaji we jaribu kulitamka tu kichwani neno "mama wa kambo" kisha uniambie inavyosound.
Mama wa kambo anaface changamoto nyingi sana akiwa anaishi na mtoto asiye wake mi nimemuona aunt yangu imefikia point anashindwa hata kuwafokea watoto wa uncle kisa tu anaogopa watahisi yote hayo kwa sababu mama yao hayupo Aunt anabaki anaumia tu pale akiona makosa yakifanywa na watoto hao hali hii imefanya awe anamuadhibu mtoto wake tu hadi kupelekea mtoto wake ajione kama yeye ndo apendwi pale kwa aunt.Kwa kweli hali hii inaleta mvurugano kwenye malezi na hata mapenzi kwa ujumla
NB;Kama unaweza liepuke kabisa kuliko kutaka kujaribu.
 
Kulea mtoto wa mtu ni kazi lakini kama imeshatokea inabidi ufanye maamuzi ya hekima
Kama umempenda mwenzio inabidi na wanae kuwapenda na kuwajenga katika misingi mizuri
Ingawa ni ngumu jamani
Unaweza fanya jema likaonekana baya
 
Mimi niko tayari kwa mtoto mmoja tu na sio zaidi tena nimlee tangu akiwa mdogo sio mkubwa na mama yake awe ameshaolewa na mtu mwingine!
 
Mie nimeolewa nikamkuta mumewangu anawatoto wawili wamechwa na mama yao wakiwa na umri wa miaka3 na mwengine miezi 10 na sababu kubwa nilikua nawaonea huruma wale watoto vp mwanamke unagua na moyo wa kiume kumuachia mwanamme watoto wako wadogo sababu anasema atalijua jiji,leo hii watoto wako 16 na 13yrs nawapenda sana na watoto wangu wanajua kama wale ni dada na kaka yao wa kwanza na sijawambia kama sio mama mmoja,mama yao watoto nilimpigia cm nikamwambia njoo uwaone watoto alinambia usione raha yakulala na baba yao ujue na raha yakulea pia unao hao nilishangaaa! lakini nimezowea na maisha yanakwenda,sasa ukipenda boga upende na majani yake...
 
kuishi na watoto sio kazi ...
tatizo linakuja kama mama yao yupo hai-atakuwa anawajaza ujinga cause ana majelous na wewe
ndugu...especially wa mume na mama yao-kuwachochea wasikuheshimu
baba yao-kama sio mwelewa akashindwa kuwaunganisha
hata uwe na roho ya malaika yatakushinda
 
Nimeamua kujibu kabla ya kusoma post za wengine ili nisiwe biased.

hii naonea kutokana na experience niliyoipata.

Kulea mtoto wa kambo kwa mwanamke kwanza inategemea na 'uelewa wa hali halisi' kwamba mtoto hana hatia yeyote katika mahusiano ya hao waliomleta na asihusishwe na walichofanya wazazi wake. Hii ndio huwa inapelekwa akina mama kusema nitalea mtoto kama nimemkuta naye ila kama kazaa tukiwa tumeshaoana siwezi mlea. Swali, je kuzaa kabla au baada ya ndoa kunaondoa fact kwamba huyo ni baba wa mtoto na mtoto ana haki ya kulelewa na baba yake ukizingatia makabila mengi ya kitanzania mtoto ni wajibu wa baba? Je aliyezaliwa baada ya ndoa ndio anastahili kuwa mistreated?

Kitu cha pili ni 'nafasi ya baba katika malezi ya watoto', kama baba atampa mama nafasi ya kuwalea wale watoto wa kamabo kama wake huwa inasaidia sana katika malezi. Lakini bahati mbaya sana kuna baadhi ya kina baba wana apply 'divide n rule' principle katika familia zao. Anawafanya wale watoto wa kambo kumuona mama aliyepo hana sauti kwao sababu sio wake. Hiii mara nyingi huwa inachagiwa na wanandoa kuwa na migogoro kati yao na njia anayoona baba ya kumfrustrate mkewe ni kutengeneza gap na watoto wa kambo. Lakini mwisho wa siku watoto ndio hukosa mapenzi ya pande zote tatu baba mzazi, mama mzazi na mama wa kambo.

Mtizamo wa watoto wenyewe wa kambo, hii huwa ni pale watoto wa kambo wanapokutana na mama wa kambo wakiwa wakubwa na uelewa wa kuamua nini cha kufanya. Je wanakuona ni tishio kwao? wanakuona mwenzao? Ni watu ambao mnaweza kaa pamoja na kuzungumza tofauti zenu na kutafuta suluhisho la pamoja. Hii hutokana na malezi waliyopata toka awali.
Hapa kwenye mtizamo wa watoto kama ni wakubwa kiasi chakujitambua pia aina ya malezi waliyopata mwanzo ukilinganisha na aina ya malezi unayokuja nayo. Mfano mdogo tu, labda mwanzo walikuwa huru kuwasha TV muda wowote, lakini mama wa kambo labda kazoea TV inawashwa kuanzia jioni, ni kitu kidogo lakini ni mwanzo wa mtafaruku. Je ni kwa kiwango gani na kwa muda gani (extent & Time frame ya mabadiliko) mama wa kambo anabadili life style ya familia kama kawakuta wakubwa?

Mama mzazi anaweza kuwa na nafasi yake katika malezi. Mimi kama mama wa kambo sioni mama mzazi ataniathiri vipi maana hadi watoto wanaletwa kwangu inabidi yeye na mzazi mwenzie wawe wameelewana. Mie kama mama wa kambo kazi yangu ni kuwalea wakiwa kwangu. Kama watakuwa wanaenda kwa mama yao hayo si juu yangu sana itategemea na mkataba wa hao waliozalishana.

Kwa mtazazmo wangu, ni naweza lea watoto wa kambo bila kujali wamezaliwa katika stage gani ya ndoa, iwe kabla au baada ya ndoa. Hata kama ni ngumu ila kama bado nataka kuishi na mme lazima niwalee watoto wake kama yeye anataka waje kuishi naye. Sababu kubwa hapa ni kuwa hata kama utamnyima mme kukaa na mtoto wake wa nje kisha kampata baada ya ndoa je inabadili ukweli kuwa yule ni mtoto wake? Je unadhani itamuondolea upendo wa baba na mtoto? Je ni mara ngapi atakuwa anakosa raha kisa mtoto wake hayupo ila anaogopakusema sababu ni wa nje na hii italeta/sababisha mitafaruku mingapi? Je nikijiweka katika nafasi ya mwanamme, bahati mbaya nimebeba mimba ya hawara, nikazaa, je akiniambia nimpeleke mtoto kwa baba yake nitahuzunikaje?
Bahati iliyopo kwa wanawake ni kuwa hawa watoto tunaowapata baada ya ndoa tunawachomekea wanamme bila wao kujua.
 

Huyo mama wakati anawajaza huo ujinga atakua wapi na hao watoto?
 
Kongosho niweipenda sana post yako!
 
Asabaya,ulichokifanya wakati mwingine ni vigumu kukikuta kinafanyika kwa wanawake wengine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…