Nimeamua kujibu kabla ya kusoma post za wengine ili nisiwe biased.
hii naonea kutokana na experience niliyoipata.
Kulea mtoto wa kambo kwa mwanamke kwanza inategemea na 'uelewa wa hali halisi' kwamba mtoto hana hatia yeyote katika mahusiano ya hao waliomleta na asihusishwe na walichofanya wazazi wake. Hii ndio huwa inapelekwa akina mama kusema nitalea mtoto kama nimemkuta naye ila kama kazaa tukiwa tumeshaoana siwezi mlea. Swali, je kuzaa kabla au baada ya ndoa kunaondoa fact kwamba huyo ni baba wa mtoto na mtoto ana haki ya kulelewa na baba yake ukizingatia makabila mengi ya kitanzania mtoto ni wajibu wa baba? Je aliyezaliwa baada ya ndoa ndio anastahili kuwa mistreated?
Kitu cha pili ni 'nafasi ya baba katika malezi ya watoto', kama baba atampa mama nafasi ya kuwalea wale watoto wa kamabo kama wake huwa inasaidia sana katika malezi. Lakini bahati mbaya sana kuna baadhi ya kina baba wana apply 'divide n rule' principle katika familia zao. Anawafanya wale watoto wa kambo kumuona mama aliyepo hana sauti kwao sababu sio wake. Hiii mara nyingi huwa inachagiwa na wanandoa kuwa na migogoro kati yao na njia anayoona baba ya kumfrustrate mkewe ni kutengeneza gap na watoto wa kambo. Lakini mwisho wa siku watoto ndio hukosa mapenzi ya pande zote tatu baba mzazi, mama mzazi na mama wa kambo.
Mtizamo wa watoto wenyewe wa kambo, hii huwa ni pale watoto wa kambo wanapokutana na mama wa kambo wakiwa wakubwa na uelewa wa kuamua nini cha kufanya. Je wanakuona ni tishio kwao? wanakuona mwenzao? Ni watu ambao mnaweza kaa pamoja na kuzungumza tofauti zenu na kutafuta suluhisho la pamoja. Hii hutokana na malezi waliyopata toka awali.
Hapa kwenye mtizamo wa watoto kama ni wakubwa kiasi chakujitambua pia aina ya malezi waliyopata mwanzo ukilinganisha na aina ya malezi unayokuja nayo. Mfano mdogo tu, labda mwanzo walikuwa huru kuwasha TV muda wowote, lakini mama wa kambo labda kazoea TV inawashwa kuanzia jioni, ni kitu kidogo lakini ni mwanzo wa mtafaruku. Je ni kwa kiwango gani na kwa muda gani (extent & Time frame ya mabadiliko) mama wa kambo anabadili life style ya familia kama kawakuta wakubwa?
Mama mzazi anaweza kuwa na nafasi yake katika malezi. Mimi kama mama wa kambo sioni mama mzazi ataniathiri vipi maana hadi watoto wanaletwa kwangu inabidi yeye na mzazi mwenzie wawe wameelewana. Mie kama mama wa kambo kazi yangu ni kuwalea wakiwa kwangu. Kama watakuwa wanaenda kwa mama yao hayo si juu yangu sana itategemea na mkataba wa hao waliozalishana.
Kwa mtazazmo wangu, ni naweza lea watoto wa kambo bila kujali wamezaliwa katika stage gani ya ndoa, iwe kabla au baada ya ndoa. Hata kama ni ngumu ila kama bado nataka kuishi na mme lazima niwalee watoto wake kama yeye anataka waje kuishi naye. Sababu kubwa hapa ni kuwa hata kama utamnyima mme kukaa na mtoto wake wa nje kisha kampata baada ya ndoa je inabadili ukweli kuwa yule ni mtoto wake? Je unadhani itamuondolea upendo wa baba na mtoto? Je ni mara ngapi atakuwa anakosa raha kisa mtoto wake hayupo ila anaogopakusema sababu ni wa nje na hii italeta/sababisha mitafaruku mingapi? Je nikijiweka katika nafasi ya mwanamme, bahati mbaya nimebeba mimba ya hawara, nikazaa, je akiniambia nimpeleke mtoto kwa baba yake nitahuzunikaje?
Bahati iliyopo kwa wanawake ni kuwa hawa watoto tunaowapata baada ya ndoa tunawachomekea wanamme bila wao kujua.