Uko wapi ushahidi wa tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka ya Hayati Magufuli?

Hata jiwe wakati ameigia alituambia kuwa hataki mikutano ya kisiasa ina mchelewesha kujenga nchi!!kwani tulichezewa sana!!hizo serikali zilikuwa za chama gani?na yeye alikuwa na miaka mingapi humo!!Huyo jiwe hawezi kuachwa kamwe kuna unyama mwingi sana umefanyika kipindi chake kuliko rais yoyote yule toka tupate uhuru.MUNGU FUNDI
 

Aliweza kukujibu ...?
 
Actually ni hakuna. Hiki unachokiona sasa ni focus shifting ili wampe mama aupige mwingi so incompetency ya mama inafichwa kwa kumponda Magufuli.
na hawatofanikiwa kwa hicho wanachokifanya maana wanatumia nguvu nyingi sana kumponda lakini bado sifa zinamuangukia
 
Hii ni kweli 100%👉Wabongo wanapenda umbea na Majungu jambo alisikia analibeba moja kwa moja kwenye mitandao ila ukimuuliza swali utaishia kutukanwa tu maana hakuna analojua, muulize ushahidi juu ya tuhuma za Magufuli abakia alisikia, aliambiwa, watu wanasemaga, kuna story hiyo, kuna mwana alimwambia, alisoma facebook na instagram, kuna mshua alimtonya, kuna demu wa town alimsikia, kuna wana wanasema, kuna ubuyu alilishwa, kiufupi hana anachojua zaidi ya Majungu tu.👈

Kama wana data watupe,vinginevyo waache uongo,majungu na umbea.
 
Kitendo Cha kununua wanasiasa wa upinzani kwa kodi za wananchi, Kisha kuitisha uchaguzi ambao tayari mshindi amepangwa, ilikuwa ni ufisadi mkubwa kuliko ufisadi wa Richmond na EPA.
Kwa maana hiyo Upinzani ina viongozi malaya ndio maana wananunulika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…