Uko wapi ushahidi wa tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka ya Hayati Magufuli?

Uko wapi ushahidi wa tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka ya Hayati Magufuli?

Tulipofika kila kiongozi anajitetea kwa wananchi kuwa anaijenga upya taasisi aliyopewa (upuuzi mkubwa huu) kila mmoja ukimuuliza atakwambia maika saba ya Magufuli hakukuwa na lolote lililofanyika, mnatuona wajinga sio?

Makamba anajenga upya njia za umeme, Mchechu anajenga upya NHC, Zitto upya ACT Wazalendo, Chongolo anaijenga upya CCM, Samia anaijenga upya serikali na ikulu, hata wale ambao bado walikuwa na Magufuli wameondolewa ili waje wangine wajenge upya!

Kila anayeulizwa amefanya nini tangu ateuliwe anasema alikuta hali mbaya sana kuanzia Rais Samia, mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya na taasisi, uongo mkubwa sana huu.

Wabongo wanapenda umbea na Majungu jambo alisikia analibeba moja kwa moja kwenye mitandao ila ukimuuliza swali utaishia kutukanwa tu maana hakuna analojua, muulize ushahidi juu ya tuhuma za Magufuli abakia alisikia, aliambiwa, watu wanasemaga, kuna story hiyo, kuna mwana alimwambia, alisoma facebook na instagram, kuna mshua alimtonya, kuna demu wa town alimsikia, kuna wana wanasema, kuna ubuyu alilishwa, kiufupi hana anachojua zaidi ya Majungu tu.

Walikuwa chini ya Magufuli wapi kama waliagizwa waseme, wakamatwe wapelekwe mahakamani maana wapo mpo nao serikalini mnashi nao, tuache yule mzee apumzike kwa amani.

USSR
Hata jiwe wakati ameigia alituambia kuwa hataki mikutano ya kisiasa ina mchelewesha kujenga nchi!!kwani tulichezewa sana!!hizo serikali zilikuwa za chama gani?na yeye alikuwa na miaka mingapi humo!!Huyo jiwe hawezi kuachwa kamwe kuna unyama mwingi sana umefanyika kipindi chake kuliko rais yoyote yule toka tupate uhuru.MUNGU FUNDI
 
Hivi ni ujinga au ni kulinda legacy?magufuli kutokuwa signatory ndio barrier kwamba hangeweza kuwa mwizi? Simply, hata nyumbani kwako chakula unachokula lazima we ndio uwe mpishi? Unapopinga hakuwa mwizi, we unaweza kuthibitisha hakuiba? Unapoambiwa viongozi wa Afrika wanaiba pesa kwao na kuficha ughaibuni, kwani huwa wanafanya personally?
Tunachotakiwa kufanya sio kupingwa hizi taarifa, bali kuunganisha nguvu kuzichunguza, hatimaye tuweze kurejesha fedha zilizoibwa na yeyote na kufichwa popote pale nchini au nje.

Aliweza kukujibu ...?
 
Actually ni hakuna. Hiki unachokiona sasa ni focus shifting ili wampe mama aupige mwingi so incompetency ya mama inafichwa kwa kumponda Magufuli.
na hawatofanikiwa kwa hicho wanachokifanya maana wanatumia nguvu nyingi sana kumponda lakini bado sifa zinamuangukia
 
Tulipofika kila kiongozi anajitetea kwa wananchi kuwa anaijenga upya taasisi aliyopewa (upuuzi mkubwa huu) kila mmoja ukimuuliza atakwambia maika saba ya Magufuli hakukuwa na lolote lililofanyika, mnatuona wajinga sio?

Makamba anajenga upya njia za umeme, Mchechu anajenga upya NHC, Zitto upya ACT Wazalendo, Chongolo anaijenga upya CCM, Samia anaijenga upya serikali na ikulu, hata wale ambao bado walikuwa na Magufuli wameondolewa ili waje wangine wajenge upya!

Kila anayeulizwa amefanya nini tangu ateuliwe anasema alikuta hali mbaya sana kuanzia Rais Samia, mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya na taasisi, uongo mkubwa sana huu.

Wabongo wanapenda umbea na Majungu jambo alisikia analibeba moja kwa moja kwenye mitandao ila ukimuuliza swali utaishia kutukanwa tu maana hakuna analojua, muulize ushahidi juu ya tuhuma za Magufuli abakia alisikia, aliambiwa, watu wanasemaga, kuna story hiyo, kuna mwana alimwambia, alisoma facebook na instagram, kuna mshua alimtonya, kuna demu wa town alimsikia, kuna wana wanasema, kuna ubuyu alilishwa, kiufupi hana anachojua zaidi ya Majungu tu.

Walikuwa chini ya Magufuli wapi kama waliagizwa waseme, wakamatwe wapelekwe mahakamani maana wapo mpo nao serikalini mnashi nao, tuache yule mzee apumzike kwa amani.

USSR
Hii ni kweli 100%👉Wabongo wanapenda umbea na Majungu jambo alisikia analibeba moja kwa moja kwenye mitandao ila ukimuuliza swali utaishia kutukanwa tu maana hakuna analojua, muulize ushahidi juu ya tuhuma za Magufuli abakia alisikia, aliambiwa, watu wanasemaga, kuna story hiyo, kuna mwana alimwambia, alisoma facebook na instagram, kuna mshua alimtonya, kuna demu wa town alimsikia, kuna wana wanasema, kuna ubuyu alilishwa, kiufupi hana anachojua zaidi ya Majungu tu.👈

Kama wana data watupe,vinginevyo waache uongo,majungu na umbea.
 
Kitendo Cha kununua wanasiasa wa upinzani kwa kodi za wananchi, Kisha kuitisha uchaguzi ambao tayari mshindi amepangwa, ilikuwa ni ufisadi mkubwa kuliko ufisadi wa Richmond na EPA.
Kwa maana hiyo Upinzani ina viongozi malaya ndio maana wananunulika
 
Back
Top Bottom