Ukoloni unarudi Tanzania?

we tapeli huna unachojua, kwanza ole Mushi ndio jina gani.
 
Ndoto ya mchana ccm kuwatoa kwa njia ya ballot.
Sijawahi kukata tamaa na njia ya ballot. 2014-2015 ilibidi wapige magoti haswa....

2024-2025 hata wakitoa machozi ya kenge jibu liwe hapana[X] kuwaondoa hawa waliopo madarakani inawezekana kabisa.

CCM can be revived and cleaned Inside out. Believe me.
 
Tuchague lakini upinzani!
Haswa, ikiwa tunaweza lete upinzani ndani kuja nje, vilevile kuungana na wote wapenda NCHI. Hakika muungano wetu(sio 64) unaweza kuleta mabadiliko makubwa Nchini.

CCM hii hii inaweza kurudi, minus madubwana na madubwasha yaliyomo.
 
Sijakubishia mkuu ila sio kwanjia ya ballot amini nachokuambia hawa wanatakiwa kuwatoa kwanjia ya maandamano nchi mzima na kumuwela Lisu pale ikulu.
 
Hawa Kenge si ndio machawa wa Makonda waeneza propaganda eti Makonda kateuliwa kuwa Katibu Mwenezi wa Ccm badala ya Sofia Mjema.

Kuna watu akiwemo huyu mpuuzi Ole Mushi wamemisi kunywa damu za watu sasa wameanzisha propaganda kubwa kumpigia debe yule shetani Bashite.
 
WANACCM WOTE KWA UJUMLA WETU TUNAUNGA MKONO SUALA LA UWEKEZAJI WA DP WORLD TANZANIA,MTUNZI WA ARTICLE HII, JISEMEE KWA NAFSI YAKO!
KIGOGO WA CCM NA SERIKALI ATOA MAONI JUU YA MKATABA WA BANDARI KUPITIA KWA ASKOFU ILI ASIFUKUZWE UANACHAMA!

Ujumbe ufuatao umetoka kwa mwanachama wa CCM ambaye amekuwa Mteule wa Rais wa muda mrefu. Kwa kuogopa kufukuzwa CCM, ameomba afikishe ujumbe kupitia kwa Askofu.

Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!
Kwenye vikao vilivyoisha (Kamati Kuu ya CCM na Halmashauru Kuu ya CCM) imeelezwa kuwa Wajumbe wamebariki mkataba tata wa Bandari. Ninajiuliza maswali kadhaa: Je, ni Wajumbe wangapi katika vikao hivyo ni wanasheria au wachumi walioweza kuingia katika vikao na nakala ya mkataba na kuanza kujenga hoja ya kujadili kifungu kwa kifungu kuwa kifungu hiki hakiko sawa na hiki kiko sawa?

Je, Mwenyekiti wa kikao alitangaza maslahi yake katika jambo husika kuona busara kuwa jambo hilo lijadiliwa kwa uwazi bila yeye kuwa Mwenyekiti wa kikao kwa kuwa limepigiwa kelele sana na hivyo kujenga neutrality kwake? Je, isingekuwa ni busara kumuachia Makamu Mwenyekiti ili asimamie vikao husika?

Mpendwa Baba Askofu! Unajua kwenye Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ili mtu aweze kuingia katika Political Committee ama Kamati ya Siasa na ngazi zingine kubwa za maamuzi ni lazima awe na uelewa wa mambo hususani katika masuala ya fedha, sheria, mazingira na pia lazima awe na elimu au uwezo wa kuweza kujenga hoja.

Je ni Wajumbe wangapi katika vikao vyetu ambao ni wanasheria na wachumi walio na uwezo wa kujenga hoja katika vikao ambavyo tumeambiwa kuwa wameridhia kwa kishindo?

Ninaomba ikikupendeza Baba Askofu unisaidie kuyafikisha haya kwa Watanzania kwani sio wote ndani ya CCM tunaounga mkono mkataba huo wa Bandari. Mazingira yetu ni magumu na hivyo tunaogopa kufukuzwa uanachama ndio maana hatutoki hadharani kupinga au kukosoa.

Ndimi .....
Dar es Salaam, 10 Julai 2023
 
Posta imetolewa Kwa mwarabu?
Ushirikiano nao ni kutoa?
Kwahiyo nchi zote tunazo shirikiana ni tunawapa?...
Akili za wapi hizi?
At what percentage ukitoa more than 50% wewe sio tena unayeshirikisha bali unashirikishwa... (na kama kama asset ilikuwa yako in the beginning - hio ni another definition ya kupigwa) Na upigaji huu unatokea sio kwamba wanaoingia mikataba hawajui bali wanajali 10% zao kuliko long term welfare ya Nchi zao)

Solution ni Transparency tu..., tujue ni nini wanafanya hawa walinzi wa mali zetu waliogeuka kuwa walafi wa mali zetu (Ni kama kumpa ngedere akulindie shamba la mahindi alafu wewe mkulima usiruhusiwe kuangalia kinachoendelea)
 
Bora ya wakoloni wa awali kuliko ccm na wakoloni wa Sasa kama wawekezaji
 
Hata tukawachagua CHADEMA ni hayo hayo tu. Kitachofanyika ni kuwatoa hao uliowataja na kuwaleta Wabelgiji. Hatuna ujanja, tumebanwa vizuri.
69 milioni, yes tumeshindwa kuchaguana. Alternative tulizonazo ni Dr Slaa (Muongo mkubwa), Lissu (mropokaji, kichwa maji + Mbelgiji). Hatuna pakukimbilia ndugu yangu.
 
Kwa hiyo umekubali hata mwarabu akiamua kukulamba utakubali tuu kwa vile huna pa kukimbilia?
Unajitangazia unyonge bila aibu?
 
Kwa hiyo umekubali hata mwarabu akiamua kukulamba utakubali tuu kwa vile huna pa kukimbilia?
Unajitangazia unyonge bila aibu?
Rafiki yangu neno kutawaliwa kwa maana hii nyie mnayeitoa, haipo nchi afrika iliyokuwa na uhuru huo unaoufikiria.
Sasa hivi nyie mnapiga kelele huku mkimuunga Dr Slaa na Lissu bila kujua kuwa kwa kuwaunga mkono hao mnawakaribisha Wabelgiji/ Magu alikuwa anawaita mabwana zao. Napenda kurudia, ninapenda mjue mnachofanya, msije mkaanza harakati nyingine kwa kutokujua mkifanyacho sasa hivi.
 
Mbona posta inashirikiana na Makampuni mengi Tu ya Ulaya?
Nashauri punguza islamophobia na stereo types ...

Ushirikiano siku zote unaamua wewe kipi ushiriki kipi ukatae...sio mkataba wa kununua wala kukodisha...
Samahani mkuu
Unaundugu na @feizafox?
Maana wote hamna hoja zaidi ya udini
 
Sijui kama hats unachoandika hapa we mwenyewe unakielewa!
Anyway, tutafika tuu
 
Sijui kama hats unachoandika hapa we mwenyewe unakielewa!
Anyway, tutafika tuu
Na hiyo anyway....... ndicho nilichokuwa namaanisha. Ni kweli tutaelewana tu na tutafika tuu. Nisiandike mengi, jibu lako linatosha.
 
😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…