Ukoloni unarudi Tanzania?

Ukoloni unarudi Tanzania?

Asante mkuu. Umeandika vizuri. Ni shida mnoo kuwa na mawazo ya kutokupambana. Huu ni uvivu wa hali ya juu. Yaani ukikwama kidogo tu unawaza kukopa, kuomba, kusaidiwa, kuiba. Hii ni shida sana kushindwa kujisimamia.
Mkuu Mimi nimeikopi na kuiweka hapa
 
Thadei Ole Mushi ni mnafiki mmoja tu.
 
Asante mkuu. Umeandika vizuri. Ni shida mnoo kuwa na mawazo ya kutokupambana. Huu ni uvivu wa hali ya juu. Yaani ukikwama kidogo tu unawaza kukopa, kuomba, kusaidiwa, kuiba. Hii ni shida sana kushindwa kujisimamia.
"Blacks are born with an a half-mad mindsets and shelf esteems".
By Jan Smuts.

Aidha, watu weusi wengi zaidi duniani wanaishi kwa kutegemea BAHATI NASIBU na MIUJIZA, wakati watu wa races zingine wanaishi kwa kutegemea ELIMU, MIPANGO, na MIKAKATI MADHUBUTI katika nyanja zote za maisha yao.
 
Posta imetolewa Kwa mwarabu?
Ushirikiano nao ni kutoa?
Kwahiyo nchi zote tunazo shirikiana ni tunawapa?...
Akili za wapi hizi?
We umeshirikishwa huko kwao hao unaoshirikiana nao? Ushirka wa wapi upo upande mmoja tu?

Africa tuache ujinga, huwezi kuwa partner kama haupo level moja na unaoshirikiana nao, hiyo ni parasitic mode of relationship haiwezi kuwa symbiotic.

Na uhakika kabisa wewe ni mfaidika wa mfumo huu dhalili ndiyo sababu huoni wala husiki. Na tabia ya watu kama wewe ni pale favour inapoondoka ndipo mnaanza kudhani ndiyo unahaki ya kutumia akili.

Ninyi wa hivi ndiyo chawa wenyewe ambao mwandishi anawazungumzia, sawa na wale matarishi wa enzi za ukoloni. Nonyi wa mentality hii niwakuogopwa kama ukoma.

tunaanza campaign ya kuwadhibiti watu wenye mawazo kama yako.
 
Mbona posta inashirikiana na Makampuni mengi Tu ya Ulaya?
Nashauri punguza islamophobia na stereo types ...

Ushirikiano siku zote unaamua wewe kipi ushiriki kipi ukatae...sio mkataba wa kununua wala kukodisha...
 
Aise! Wewe kati ya yooote umeona uislam, hivi hujui kuwa mimi ni muislam ama?

Mwislamu hana shirki kama zako, unaoufanya hapa ni shirk wala si dini hii...Acha laana ndugu yangu, muislam safi hawi na ubaguzi kama wako anajua maana ya dhambi
 
Wewe Acha uongo...
Tuna miakataba ya ushirikiano na Japan...je tuko level moja na Japan??

Punguza islamophobia....mkiona mwarabu Tu mnawaza uovu ambao haupo...sasa posta kushirikiana na Oman kuna shida gani?
Wewe unajua Posta Wana mikataba mingapi ya kushirikiana?
 
Wanashiriki kwenye kampuni gani nikumbushe ya umma tena nyeti kama hizo...
 
Na Thadei Ole Mushi

Miaka 60 ya Uhuru tumeshindwa kabisa kusimamia rasilimali zetu wenyewe.

Migodi tumeitoa kwa Wazungu, Misitu tumeitoa kwa Mwarabu, Posta tumeitoa kwa Mwarabu, Misitu tumeitoa kwa mwarabu, Gesi tumeitoa kwa Mzungu, Uwanja wa ndege wa KIA nao tumeutoa, TPDC tumeitoa, Bandari tumeitoa kwa mwarabu, Loliondo tumeitoa kwa Mwarabu, karibi maeneo yote Muhimu tumeshatoa…. Sisi tumebakia na nini?

Maswali ni Mengi mno….

1. Tulidai Uhuru wa Nini?

2. CCM imeshindwa kuiongoza Nchi? Maana kila eneo tuliloliwekeza tunasema kuna wapigaji hivyo bora tumpe mwekezaji. Je Serikali ni dhaifu imeshindwa kuzuia upigaji?

3. Vyuo Vikuu zaidi ya 31 nchini vimeshindwa kutengeneza wasomi wa kusimamia hizi rasilimali za taifa? Kazi za Graduate wetu kubwa ni kuendesha Bodaboda, kama taifa tunajua tunakoelekea?

4. Tanzania tunaweza jambo gani kubwa hapa nchini? Mambo yote ya muhimu tunaona ni Magumu tunawapa wawekezaji je sisi ni kitu gani tunaweza? Wenzetu wanawezaje sisi tunashindwa? Huu uvivu wa kufikiri tumeutoa wapi?

5. Baada ya Bandari tunaenda kuwekeza rasilimali gani tena? Ukiona wabunge wetu wanavyovaa Suti Pale Bungeni na taifa linapoelekea utatamani kulia. Hawa watu (wabunge) tunawalipa mishahara, tunawanunulia mafuta ya magari, watoto wao tunawasomesha na bado wanatuibia kupitia mikataba hivi nani alituloga tukawa waoga hivi?

6. Tanzania ya watu Milioni 69 plus tumeshindwa kuchaguana miongoni mwetu tupate watu wanaoweza kutuvusha hapa tulipo kwa kuwa taifa linaelekea kutawaliwa kwa mara ya Pili?

7. Wakati Uganda ilipogundua kuwa ni kweli Taifa lao lina mafuta walichukua vijana wao wakakimbiziwa ughaibuni kwenda kujifunza kuhusu Oil Production na asilimia kubwa ya mradi wao wa mafuta ni vijana wanausimamia. Sisi badala ya kuandaa vijana tunatuma kina Steve Nyerere na kina Kitenge kwenda kukagua Bandari za wenzetu hivi nani alituloga?

8. Vijana asilimia 90 sasa hivi hapa nchini bila kujali elimu zao kazi zao kubwa za kujipatia kipato ni Kubet au kuendesha Bodaboda. Huku maeneo muhimu ya rasilimali za taifa lao zikigawanywa kwa wazungu na waarabu kwa jina la kusema ni mwekezaji. Hii ni hatari sana kwa taifa letu…. Tanzania ina wanyamapori kila mahali ila anayekula nyama pori first class kabisa hapa Tanzania ni Mwarabu hii ni aibu…

9. Je tuliwahi kupata Uhuru? Lakini mbona Kina Singapore walipata Uhuru nyuma yetu? Mbona leo ipo mbali sana na wanajisimamia wenyewe?

10. Hata kuzalisha mafuta ya kula ya kutosha kwa taifa zima tumeshindwa tunaagiza nje ya nchi, Ngano tunaagiza, Mbolea tunaagiza, Maziwa ya Unga na hata ya kawaidia tunaagiza, pale Bandarini asilimia 95 ni bidhaa zinaingia nchini badala ya kutoka hivi tunaelekea wapi?

CCM ikubali sasa kutumia watu ambao wapo nje ya familia zenye Connection kwenye Uongozi wa nchi hii. Babu alikuwa kiongozi, mtoto akatafutiwa connection akawa kiongozi, mjukuu naye akawa kiongozi nk …. Hizi DNA kwa mazingira ya Sasa zimechoka au CCM ikubali kuwaachia wengine wajaribu kutusogeza tulipo.

Kuna siku nilisema kama Africa itaheshimu Sanduku la Kura katika kuchaguana tutafika mbali sana. Na kama askari polisi wa Mataifa ya Africa watatimiza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria hili bara linapiga hatua kubwa. Askari anamlinda mtu mwenye V8, Mke ana gari, watoto wa huyo Mtu wanachukuliwa na School Bus wanakupita getini unawachekelea kama Zuzu, huku kwako ukiwa unafukuzana na Baba Mwenye nyumba anakudai kodi, kijana wako wa kwanza aliyehitimu Chuo kikuu anashinda vibanda umiza anabet, wanao wanasoma shule za makabwela kabisa huku akiwa hana uniform za kubadilisha lakini bado unaendelea kupiga Salute kwenye mageti ya viongozi.

Vijana kwa Rasilimali zilizopo hapa nchini hampaswi kukesha mkiwa mna Bet na kuendesha Boda boda. Wafanyakazi kwa rasilimali zilizopo Hampaswi kulipwa mishahara mnayolipwa. Hivyo basi watu kama kina Steve Nyerere na kina Maulid Kitenge ni wa kuwatenga kwenye jamii yetu…. Tunatakiwa tuanze kutokomeza hizi chawa kwanza kabla hatujawafikia Viongozi wetu.

Wakati ukoloni ukibisha Hodi Africa ulikuja kwa njia ya Mikataba. Ndiko tunakoelekea…..

Vijana tuliopo ndani ya CCM ni wakati wa kujitafuta sasa tuache kusifia ujinga wakati taifa limekwama. Tuzungumze, tukatae kabisa kuwa Chawa wa mtu, wakati ni sasa….. kila mtu kwenye familia yake atoe elimu ya Uraia.

Tumekwama kama Taifa….. share

Ole Mushi
0712702602
Kwani ulikwenda wapi? Ukoloni haujawahi kutoka Afrika ikiwemo Tanzania. Uwe ni wa kutoka uingereza, ufaransa, Urusi, Uturuki, Vatkan, Qatar n.k, lakini haujatoka bali unabadili majina tu.
Ukamwita Bebari au muwekezaji ni juu yako, yeye kanuni zake ni zile zile utabadilika wewe.
Ole Mushi usitudanganye na degree, phd au cheti cha historia.
 
Posta imetolewa Kwa mwarabu?
Usiwe mjinga wewe...baada ya CCM kuitangazia dunia kwamba hakuna Mtanzania hata moja mwenye sifa, uwezo wala uadilifu wa kusimamia kilicho chetu, ulitegemea nini?
Ushirikiano nao ni kutoa?
Kuwa japo na akili...baada ya CCM kuitangazia dunia kwamba Watanzania kwa ujumla wetu ni walafi, wadokozi na wezi, mjinga gani huyo yuko tayari kushirikiana nasi?
Kwahiyo nchi zote tunazo shirikiana ni tunawapa?...
Ndio, tunawapa kwa kuwa ni Utawala wa CCM, sera za CCM na uongozi wa CCM ndio umetufikisha hapo na kibaya zaidi kwa ubabe wameng'ang'ania madaraka.
Akili za wapi hizi...
Ni akili za CCM. Adui wa taifa hili ni CCM kwani mtaji wa CCM ni ujinga, pumzi ya CCM ni unafiki, misingi ya CCM ni matumizi ya nguvu kulinda itikadi yao ya kifisadi.

CCM yaipakata D world!.jpeg

Arab_slavers.jpg
 
Pamoja na kwamba hatuna uthibitisho wa kila kilichotajwa hapa,
ni kweli kwamba kuna tatizo kubwa katika fikra na mtazamo wa jumla kuhusu kuendeleza watu wetu na taifa kiuchumi.
Maamuzi ya Utegemezi na udalali wa raslimali za taifa kwa jina la uwekezaji yanapaswa kutazamwa upya.
Jambo la msingi kwa viongozi ni kuelewa kwamba, nchi hujengwa na wananchi wenyewe na kamwe siyo wageni.
Wageni huwekeza ili wakajenge nchi zao.
Hii Imani ya hatuwezi tuwape wawekezaji kila kitu itaua taifa baada ya asilimia kubwa ya raia kuwa watumwa wa kisasa.
 
Wewe Acha uongo...
Tuna miakataba ya ushirikiano na Japan...je tuko level moja na Japan??

Punguza islamophobia....mkiona mwarabu Tu mnawaza uovu ambao haupo...sasa posta kushirikiana na Oman kuna shida gani?
Wewe unajua Posta Wana mikataba mingapi ya kushirikiana?
Kwa hiyo posta ufanisi tunao? Tuiache tusibinafsishe
 
Usiwe mjinga wewe...baada ya CCM kuitangazia dunia kwamba hakuna Mtanzania hata moja mwenye sifa, uwezo wala uadilifu wa kusimamia kilicho chetu, ulitegemea nini?

Kuwa japo na akili...baada ya CCM kuitangazia dunia kwamba Watanzania kwa ujumla wetu ni walafi, wadokozi na wezi, mjinga gani huyo yuko tayari kushirikiana nasi?

Ndio, tunawapa kwa kuwa ni Utawala wa CCM, sera za CCM na uongozi wa CCM ndio umetufikisha hapo na kibaya zaidi kwa ubabe wameng'ang'ania madaraka.

Ni akili za CCM. Adui wa taifa hili ni CCM kwani mtaji wa CCM ni ujinga, pumzi ya CCM ni unafiki, misingi ya CCM ni matumizi ya nguvu kulinda itikadi yao ya kifisadi.
CCM kama ideology ni chama imara na kizuri tatizo hao wachache wanaotaka kuijibinafsisha kwa manufaa binafsi ndiyo shida...Usituhusishe wana CCM wote kwakua ndiyo sisi sisi wakulima na wafanyakzi watanzania walipa kodi namba moja nchi hii, japo mafisadi wanatutumia kwa faida binafsi na kutuchafulia chama chetu.

Unapoitaja CCM wakumbuke founders wetu Karume, Nyerere, Sykes, Bibi Titi etc linganisha hao watu na ukoo wao na wale wapigania uhuru wa nchi zingine ambao walijimilikisha utajiri wa nchi zao baada ya uhuru...Niambie Makongoro leo si ndiyo anagekuwa ana own bandari kama siyo CCM aliyoianzisha baba yake? Lisu leo angekuwa mchunga ng'ombe huko kwao etc. Usiifananishe CCM na watu waajabu ajabu...Hao wanaitumia CCM kama koti tu kujipa joto binafsi na familia zao
 
Posta imetolewa Kwa mwarabu?
Ushirikiano nao ni kutoa?
Kwahiyo nchi zote tunazo shirikiana ni tunawapa?...
Akili za wapi hizi?
Umeisoma mikataba yenyewe? Ni kama huu tu wa Bandari
 
UKOLONI UNARUDI TANZANIA?

Na Thadei Ole Mushi.

Miaka 60 ya Uhuru tumeshindwa kabisa kusimamia rasilimali zetu wenyewe.

Migodi tumeitoa kwa Wazungu, Misitu tumeitoa kwa Mwarabu, Posta tumeitoa kwa Mwarabu, Misitu tumeitoa kwa mwarabu, Gesi tumeitoa kwa Mzungu, Uwanja wa ndege wa KIA nao tumeutoa, TPDC tumeitoa, Bandari tumeitoa kwa mwarabu, Loliondo tumeitoa kwa Mwarabu, karibi maeneo yote Muhimu tumeshatoa…. Sisi tumebakia na nini?

Maswali ni Mengi mno….

1. Tulidai Uhuru wa Nini?

2. CCM imeshindwa kuiongoza Nchi? Maana kila eneo tuliloliwekeza tunasema kuna wapigaji hivyo bora tumpe mwekezaji. Je Serikali ni dhaifu imeshindwa kuzuia upigaji?

3. Vyuo Vikuu zaidi ya 31 nchini vimeshindwa kutengeneza wasomi wa kusimamia hizi rasilimali za taifa? Kazi za Graduate wetu kubwa ni kuendesha Bodaboda, kama taifa tunajua tunakoelekea?

4. Tanzania tunaweza jambo gani kubwa hapa nchini? Mambo yote ya muhimu tunaona ni Magumu tunawapa wawekezaji je sisi ni kitu gani tunaweza? Wenzetu wanawezaje sisi tunashindwa? Huu uvivu wa kufikiri tumeutoa wapi?

5. Baada ya Bandari tunaenda kuwekeza rasilimali gani tena? Ukiona wabunge wetu wanavyovaa Suti Pale Bungeni na taifa linapoelekea utatamani kulia. Hawa watu (wabunge) tunawalipa mishahara, tunawanunulia mafuta ya magari, watoto wao tunawasomesha na bado wanatuibia kupitia mikataba hivi nani alituloga tukawa waoga hivi?

6. Tanzania ya watu Milioni 69 plus tumeshindwa kuchaguana miongoni mwetu tupate watu wanaoweza kutuvusha hapa tulipo kwa kuwa taifa linaelekea kutawaliwa kwa mara ya Pili?

7. Wakati Uganda ilipogundua kuwa ni kweli Taifa lao lina mafuta walichukua vijana wao wakakimbiziwa ughaibuni kwenda kujifunza kuhusu Oil Production na asilimia kubwa ya mradi wao wa mafuta ni vijana wanausimamia. Sisi badala ya kuandaa vijana tunatuma kina Steve Nyerere na kina Kitenge kwenda kukagua Bandari za wenzetu hivi nani alituloga?

8. Vijana asilimia 90 sasa hivi hapa nchini bila kujali elimu zao kazi zao kubwa za kujipatia kipato ni Kubet au kuendesha Bodaboda. Huku maeneo muhimu ya rasilimali za taifa lao zikigawanywa kwa wazungu na waarabu kwa jina la kusema ni mwekezaji. Hii ni hatari sana kwa taifa letu…. Tanzania ina wanyamapori kila mahali ila anayekula nyama pori first class kabisa hapa Tanzania ni Mwarabu hii ni aibu…

9. Je tuliwahi kupata Uhuru? Lakini mbona Kina Singapore walipata Uhuru nyuma yetu? Mbona leo ipo mbali sana na wanajisimamia wenyewe?

10. Hata kuzalisha mafuta ya kula ya kutosha kwa taifa zima tumeshindwa tunaagiza nje ya nchi, Ngano tunaagiza, Mbolea tunaagiza, Maziwa ya Unga na hata ya kawaidia tunaagiza, pale Bandarini asilimia 95 ni bidhaa zinaingia nchini badala ya kutoka hivi tunaelekea wapi?

CCM ikubali sasa kutumia watu ambao wapo nje ya familia zenye Connection kwenye Uongozi wa nchi hii. Babu alikuwa kiongozi, mtoto akatafutiwa connection akawa kiongozi, mjukuu naye akawa kiongozi nk …. Hizi DNA kwa mazingira ya Sasa zimechoka au CCM ikubali kuwaachia wengine wajaribu kutusogeza tulipo.

Kuna siku nilisema kama Africa itaheshimu Sanduku la Kura katika kuchaguana tutafika mbali sana. Na kama askari polisi wa Mataifa ya Africa watatimiza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria hili bara linapiga hatua kubwa. Askari anamlinda mtu mwenye V8, Mke ana gari, watoto wa huyo Mtu wanachukuliwa na School Bus wanakupita getini unawachekelea kama Zuzu, huku kwako ukiwa unafukuzana na Baba Mwenye nyumba anakudai kodi, kijana wako wa kwanza aliyehitimu Chuo kikuu anashinda vibanda umiza anabet, wanao wanasoma shule za makabwela kabisa huku akiwa hana uniform za kubadilisha lakini bado unaendelea kupiga Salute kwenye mageti ya viongozi.

Vijana kwa Rasilimali zilizopo hapa nchini hampaswi kukesha mkiwa mna Bet na kuendesha Boda boda. Wafanyakazi kwa rasilimali zilizopo Hampaswi kulipwa mishahara mnayolipwa. Hivyo basi watu kama kina Steve Nyerere na kina Maulid Kitenge ni wa kuwatenga kwenye jamii yetu…. Tunatakiwa tuanze kutokomeza hizi chawa kwanza kabla hatujawafikia Viongozi wetu.

Wakati ukoloni ukibisha Hodi Africa ulikuja kwa njia ya Mikataba. Ndiko tunakoelekea…..

Vijana tuliopo ndani ya CCM ni wakati wa kujitafuta sasa tuache kusifia ujinga wakati taifa limekwama. Tuzungumze, tukatae kabisa kuwa Chawa wa mtu, wakati ni sasa….. kila mtu kwenye familia yake atoe elimu ya Uraia.

Tumekwama kama Taifa….. share

Ole Mushi
0712702602
 
Nukuu:
Askari anamlinda mtu mwenye V8, Mke ana gari, watoto wa huyo Mtu wanachukuliwa na School Bus wanakupita getini unawachekelea kama Zuzu, huku kwako ukiwa unafukuzana na Baba Mwenye nyumba anakudai kodi, kijana wako wa kwanza aliyehitimu Chuo kikuu anashinda vibanda umiza anabet, wanao wanasoma shule za makabwela kabisa huku akiwa hana uniform za kubadilisha lakini bado unaendelea kupiga Salute kwenye mageti ya viongozi
 
Back
Top Bottom