Jacob Mulikuza
Member
- Jul 15, 2021
- 16
- 61
Kwenye taaluma ya ikolojia tumefundishwa kuwa, kukubali uwepo wa tatizo ni sehemu muhimu ya suluhisho ila kukana uwepo wa tatizo na kutafuta njia mbadala wa kutatua tatizo kanwa ni pata potea.
Ni ukweli kuwa matatizo mengi ya kijamii yanayohusisha mwingiliano wa mwanaume na mwanamke yanatokana kwa asilimia mia moja na mfumo dume ulioratibu matatizo haya kwa kiasi kikubwa. Mfumo dume (Male chauvinism) ni ile Imani kuwa mwanaume ni bora na mwenye uwezo mkubwa kuliko wanawake kwa maana ya akili, uwezo, nguvu na kadhalika.
Mfumo dume ni mfumo mkongwe sana unaokadiriwa kuanza kunukuliwa kwenye maandishi kuanzia miaka ya 1935. Mfumo dume uliasisiwa na jamii nyingi ili kulinda maslahi ya wanaume kwa kiasi kikubwa kwa kuwa wanaume wakati huo walikuwa kwenye nafasi za madaraka ama kufanya maamuzi.
Mfumo dume wa kila jamii uliweka misingi inayoonyesha utofauti kati ya mwanamke na mwanaume kijamii na kudogodesha utofauti wa msingi wa kibayolojia kati ya mwanamke na mwanaume. Hapa namaanisha mwanamke na mwanaume wanautofauti wa kibayolojia kwa maana ya kubeba mimba, kutungisha mimba, kunyonyesha na maumile mengine ya kimwili. Ila mfumo dume ukaweka mbali sababu hizi na kujikita kwenye sababu za mahusiano jamii kati ya mwanamke na mwanaume na kumfanya mwanamke kuwa dhaifu kwa mwanaume na kuweka vigezo kama nguvu, akili, ushujaa, ulinzi, ustahimilivu, ukakamavu na nyingine nyingi kama sifa muhimu na imara kwa mwanaume. Mfumo dume ukawapa wanawake sifa kama heshima, upendo, upole, utii na nyinginezo kama sifa dhaifu kwa wanawake.
Mfumo dume huu ukapanda ngazi kutoka kwenye tamaduni za jamii moja moja kwenda kwenye mifumo rasmi ya ajira, elimu, dini na kwingineko na kutuaminisha kuwa mwanaume ni bora kuliko mwanaume na utofauti huu ni halali katika nyanja zote muhimu.
Mfumo huu umeota mizizi kiasi kana kwamba mtu ukihoji kwanini kuna utofauti huu kati ya mwanamke na mwanaume utasikia watu wakirejea vitabu vya dini, mila na tamaduni za jamii, mifumo ya elimu na kiutawala kuhalalisha utofauti huu. Mfumo dume ni mfumo kandamizi wenye ajenda za kibaguzi kati ya mwanaume na mwanamke ulioasisiwa kwa lengo mahususi la kuwakandamiza wanawake kwa maslahi ya wanaume.
Waasisi wa mfumo dume ambao ni wanaume kwa mantiki hii, waligundua uwezo mkubwa wa mwanamke na kuogopa kuwa wadhaifu kwa wanawake hivyo kuasisi mfumo utakaowakandamiza wanawake bila wao kujua wanakandamizwa kwa kuwajengea imani kuwa hivyo ndivyo mambo yalivyo kiasili.
Na imani hii, imejengeka kwa kiasi kikubwa na tunashindwa kupata suluhisho husika tukidhani tatizo lililopo ni mwanamke na kushindwa kuona mfumo dume ulio nyuma ya matatizo haya.
Mara nyingi suluhisho la matatizo mengi yanayohusu wanawake tunaelekeza nguvu kumsaidia mwanamke badala ya kuubomoa mfumo dume unaowakandamiza wanawake.
Mfumo dume kwa kiasi kikubwa umetuaminisha ya kuwa mwanamke ni ‘KITU’ na mwanaume ni ‘MTU’ na hivyo mwanamke anatumika na mwanaume anatumia. Uhalali huu nitaueleza kwa mifano michache hapo chini.
Kwenye jamii zinazofanya ukeketaji kwa wanawake, mara nyingi tumeona suluhisho likimlenga mwanamke na kumsahau mwanaume kabisa kama sio sehemu ya tatizo. Kwa uimara wa mfumo dume, jamii hizi zimehalalisha ya kuwa mwanamke asipofanyiwa ukeketaji basi sio mwanamke kamili, hawezi kuolewa na kushiriki shughuli za kujamii.
Yaani, ukeketaji umepewa thamani zaidi kuliko utu wa mwanamke na wanawake wengi wameamini udanganyifu huu kwa imani kuwa haya ndio matakwa ya mila na tamaduni na kushindwa kuhoji kwani ukihoji utaonekana msaliti na mkosaji heshima kwenye jamii yako.
Je, tumeshawahi kujiuliza huu ukeketaji huwa unafanywa kwa maslahi ya nani? Je, wenye haja hasa na ukeketaji huu ni wanawake au wanaume?
Ukweli wa maswali haya ni kwamba, ukeketaji umeletwa kukidhi matakwa ya wanaume kwani ukeketaji unafaida kwao na si vinginevyo. Rejea mwanamke ‘kitu’na mwanaume ‘mtu’utaona kabisa mwanamke anatumika kama chombo cha kufanya mahitaji ya mwanaume yatimie.
Kwamba, mwanamke akikeketwa ataolewa (faida kwa mwanaume), mwanamke akikeketwa atatulia kwenye ndoa (faida kwa mwanaume), mwanamke akikeketwa atakuwa na heshima na atakubalika kwenye jamii (faida kwa mwanaume). Hapa utaona wazi kuwa mwanamke hana faida yoyote kwenye jamii balia anatumika kama bidhaa ya kutimiza matakwa ya wanaume.
Tuangaalie upande wa pili wa uongozi, nguvu nyingi zimewekwa kumuinua mwanamke kuwa kiongozi, kumpa fursa za uongozi, kumfanya ajiamini ataweza kuwa kiongozi na mengine mengi.
Hivi tulishawahi kujiuliza kikwazo cha mwanamke kushindwa kuwa kiongozi ni nani? Je, ni kweli mwanamke anahitaji kupewa fursa za uongozi? Je, jamii za wanawake watupu zenye viongozi nani aliwajengea uwezo wa kuwa viongozi? Je, nani alisema mwanaume ni kiongozi bora kuliko mwanamke?
Undani wa tatizo la uongozi kwa wanawake ni uongo wa mfumo dume ulituaminisha kuwa mwanaume ni kiongozi bora kuliko mwanamke na uongozi sio jukumu la kike. Mfumo dume umetumia taasisi za dini, elimu na jamii kuuhalalisha. Hapa ndio maana tunaona jitihada za kumfanya mwanamke kuwa kiongozi zinaanzia kwa wanawake badala ya wanaume kana kwamba ambao hawataki kuwa viongozi ni wanawake wakati wenye shida ni wanaume ambao hawataki mwanamke awe kiongozi na pindi akiwa watatafuta namna ya kumuangusha ili tu ashindwe.
Suluhisho pekee kwa matatizo mengi yaliyopo kwenye jamii kuanzia mimba za utotoni, ndoa, unyanyasaji wa wanawake, ukatili, uongozi, ukeketaji na mengine mengi lazima tuanza na kukubali kuwa mfumo dume ni tatizo na tuupindue mfumo dume huu kuweza kupata suluhisho.
Na kitu cha pili, jitihada zilizopo kumkomboa mwanamke zijikite kubadili fikra za wanaume kuwaona wanawake ni ‘watu’na sio ‘vitu’na kuwafanya wanaume wakubali ukweli kuwa ndio sehemu kubwa ya tatizo kwenye jamii.
Usawa wa kijinsia haupatikani kwa kuwainua wanawake badala yake kwa kuondoa imani potofu zilizojengeka kwa wanaume kuwa wanawake ni dhaifu hivyo ukombozi wa kweli uanze kwa wanaume ambao ndio sehemu ya tatizo kwenye jamii.

Upvote
24