Ukombozi kupitia masikilizano na CCM ni kupoteza muda

Ukombozi kupitia masikilizano na CCM ni kupoteza muda

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kupigania katiba nyingine ni kulenga kuleta mabadiliko kamili ya mfumo wa utawala.

IMG_20220928_112538_686.jpg

Jukumu hili ni gumu na zito kuliko kumfurusha mkoloni mlowezi halisi.

IMG_20220928_112707_292.jpg

Kwa hakika hawakukosea PAC, SA na kauli mbiu yao pendwa:

"One settler, one bullet."

Maneno matupu yakiwamo ya kuwataka wafanye hili au lile hayawezi kubadili kitu. Kwani wasipofanya itakuwa je?

IMG_20220928_125052_084.jpg

Raila anasema watu 1m wana mtosha sana. Shikamoo Fidel:

IMG_20220927_190940_421.jpg

Sisi tunataka hadi tuwe wangapi? Siyo kuwa wenye mashaka, waoga, wajinga na wa namna hiyo wapumzike tu?

NInakazia: maridhiano na wasioheshimu haki za wengine kwa maslahi gani?
 
Tuwape muda maana nia wanayo lakini mazonge yanawazonga na kuhofia kesho yao mali zao na familia zao

Kwamba Kuna wenye nia mkuu? Walamba asali hawa? Wenye kusokomezea wenzao kodi na matozo lukuki Ili wao wapate kutumbua?

IMG_20220925_111125_211.jpg

Kwamba kuna walioko huko wenye chembe ya utu au huruma? Wenye hata kutaka tu katiba iliyopo izingatiwe?

Beberu anasema "too good to be true."
 
Vipi tena mabavicha mnalialia?

Si mnapumua nyie?
 
Hakuna mtanzania wa kuwaunga mkono nyie wapinzani mlioshindwa kujenga hata ofisi ya chama na kuishia kutafuna Ruzuku zote na michango ya wabunge, Sasa Nani awape nchi nyie wababaishaji? Nyie Ni wakuongozwa Daima na siyo kuongoza nchi hii
 
Endeleeni kujifariji ila msisahau, "watu 10 au 15 tu, wanatosha sana." --asema Castro.

Nasi tunasema mwangwi wetu tu kuelekea Tahrir unatosha sana.

Kama mnadhani tunatania fikirieni tena.
 
Inashangaza, kuchekesha, au kuhuzunisha, pale unapokaa mezani na mwenzio kumueleza matatizo yako, huku yeye akiwa ndie chanzo cha matatizo hayo, anakusikiliza kwa makini na kuahidi atayafanyka kazi, lakini akitoka kikaoni anaenda kuyafanya yale maovu aliyokuahidi kuyafanyia kazi.
 
Tanzania chini ya serikali ya CCM Ni salama Sana na IPO katika mikono salama
Endeleeni kujifariji ila msisahau, "watu 10 au 15 tu, wanatosha sana." --asema Castro.

Nasi tunasema mwangwi wetu kuelekea Tahrir unatosha sana.

Kama mnadhani tunatania fikirieni tena.
 
Nimesoma weee, nimesoma kila mstari na kila neno Ila nasikitika kukuambia SIJAELEWA
 
Hakuna mtanzania wa kuwaunga mkono nyie wapinzani mlioshindwa kujenga hata ofisi ya chama na kuishia kutafuna Ruzuku zote na michango ya wabunge, Sasa Nani awape nchi nyie wababaishaji? Nyie Ni wakuongozwa Daima na siyo kuongoza nchi hii
wapo watanzania milioni2 wale mliompa lissu mwaka 2020 Kwenye uchaguzi mkuu
 
Tanzania chini ya serikali ya CCM Ni salama Sana na IPO katika mikono salama

Hata yule mfanya biashara wa mtwara aliyeporwa madini yake na wale majambazi chini ya CCM yuko salama pia?

Vipi wale wafanya biashara wa madini wa Ifakara walioporwa na majambazi chini ya uratibu wenu? Wangali salama pia?

Vipi wale watuhumiwa waliokamatwa Tarime chini ya uratibu wa CCM? Nao wangali wako salama?

Kulikoni kina Ben, Lijenje, Azory, Mawazo na wengi wengine? Mko nao wapi? Wangali salama?

Mliokuwa mnawaweka kwenye viroba nao je? Au mnadhani kila mtu kasahau?

Zingatia Tanzania ni yetu sote.

Nia yenu kumhusu Lissu ilikuwa nini?
 
Nimesoma weee, nimesoma kila mstari na kila neno Ila nasikitika kukuambia SIJAELEWA

Mwamba ndani ya wheel barrow utakiri hadharani kuelewa wewe?

IMG_20220928_112538_686.jpg

Hivi huwa mnatuona je vile?
 
Inashangaza, kuchekesha, au kuhuzunisha, pale unapokaa mezani na mwenzio kumueleza matatizo yako, huku yeye akiwa ndie chanzo cha matatizo hayo, anakusikiliza kwa makini na kuahidi atayafanyka kazi, lakini akitoka kikaoni anaenda luendeleza yale maovu aliyokuahidi kuyafanyia kazi.

Kuna lugha ambayo watu kama hawa huielewa vyema.

Tuongee nao kama wanataka, ila haki zetu kwa mujibu wa katiba hizo hazina mjadala.

Kama hawaelewi, watatukuta Tahrir.
 
Back
Top Bottom