Mchakato wa kuitoa nchi katika hatua moja duni kwenda katika hatua nyingine bora zaidi kwa jina la ukombozi, unahitaji watu waliodhamiria kweli kweli.
Jukumu hili haliwezi kuwa la kila mtu. Nyuso za watu hawa, maneno, (nyuzi, posts) na matendo yao hujionyesha.
Inawezekana namna gani kuwasikia Nyerere, Museveni, Kagame, Sokoine, Putin, Mandela, Lissu, Mbowe, Mangula, Mtikila, Seif, Malema, Garang, Saddam, Milosevic, Thatcher, Gadaffi, XI, Mengistu, Mugabe, Rawlings, Gandhi, Castro, Obama, Kim na wa namna hiyo wakiwa carried kwenye mizaha au hadithi za mbususu, simba na yanga, man city na man u, vumbi la congo na ya namna hiyo?
Pana haja ya kukatumia ka litmus haka ka kupima kudhamiria, kuwaengua wengine kwenye harakati hizi ili kutosumbuka na kupoteza muda na watu wasiojitambua.
View attachment 2374229
Kuikataa mikono yenye damu hakuwezi kuwa nusu nusu.
"Mtu hawezi kuwa mguu mmoja ndani na mwingine nje."
Ukombozi hauhitaji watu wengi. Wasanii na waachwe kuendelea na usanii wao kwa raha zao.
Ukombozi hawezi kuachiwa Mungu kutuletea bila ya sisi kuchukua hatua za makusudi.
View attachment 2374234
Ni heri kuwa na watu wachache waliodhamiria kuliko kuwa na lundo la waoga, wajinga, wapumbavu au wasaka fursa.
Ni vyema kujipima mwenyewe kutambua wewe ni asset au ni liability tukapeana nafasi kiroho safi.
Au nasema uongo ndugu zangu?