Ukombozi wa Tasnia ya filamu Tanzania

Ukombozi wa Tasnia ya filamu Tanzania

Nur boy

Senior Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
123
Reaction score
147
Kwa mwenendo wa movie za kibongo kukosa radha kwenye vitu vya uhalisia ....mimi nimeamua kula course baadae niwe na movie production ambayo itakuwa advanced na inaweza kutengeneza movie za aina zote kwa mwonekano wa uhalisia kama wazungu

Tutakuwa na uwezo wa kutengeneza movie zenye mwonekano kama wa
Avatar
Vikings
Avenger
Spider man
Black panther
Walking Dead

Zote tutatengeneza kwa viwango vya dunia
MIMI NDIO MKOMBOZI WA BONGO MOVIE
 
Filamu kali inakujaa soon Idi Amini mamaa
 
Kama umeamua kufanya hivo ni vzuri kabisa lkn isome vzuri context ya kitanzania vzuri zaidi...ili production Yako iwe context sensitive italeta Radha zaidi..kwa watazamaji..meanwhile ukimerge hizo trending production technologies
 
Sana mwanangu ndio niko nasoma maswala hayo huku naendelea na harakati za kutafuta mtaji nikianza kutoa vitu mjiandae kunipa sapoti tuu
 
Nakupongeza sana kwa dhamira yako ya kusoma na kuwekeza katika production ya filamu zenye ubora wa hali ya juu. Ni kweli kabisa filamu kubwa kama Avatar au Avengers zinaonekana kuvutia sana kwa sababu kuna kazi ya pamoja ya maelfu ya watu nyuma ya pazia, wakiwemo waandishi wa hadithi, wachoraji wa michoro ya awali (concept artists), wabunifu wa mavazi, wataalamu wa sauti, wasanii wa vionjo vya sauti, wachezaji wa nyuma (extras), na zaidi ya yote sekta nzima ya vibonzo (comics industry) inayoweka msingi wa ulimwengu wa filamu hizo.
Kwa hiyo ni kweli, mtu mmoja hawezi kubeba yote, lakini mtu mmoja anaweza kuanzisha mchakato. Kama wewe una maono, unaweza kuanza kwa kushirikiana na wachoraji wa vibonzo, waandishi wa hadithi, na wataalamu wengine. Ujenzi wa industry huanza kwa maono, mshikamano, na hatua ndogo ndogo zinazofuatana Tunahitaji wazalishaji wa maudhui kama wewe lakini pia tunahitaji kujenga mazingira yanayowakutanisha watu wa nyanja tofauti ili tufike huko pamoja
 
Kwa hakika wewe umesema ukweli kabisa ....hayo mambo yanahitaji ubunifu watu na mtaji that's why nimeanza safari na humo ndio nitaanza kutafuta yupi na yupi wanafaa kuanzia watu wa story, watu wa vibonzo, watu wa sound na editors(kipengele nyeti zaidi) kwahiyo nimejizatiti kulipambania hilo
 
Mmmmhmn,so utatumia mbinu gani ambayo wenzako saa hii hawaitumii?
 
Back
Top Bottom