Ukome tena ukome kuniita mimi mkeo balazuri mkubwa!!

Ukome tena ukome kuniita mimi mkeo balazuri mkubwa!!

nitonye

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2011
Posts
7,342
Reaction score
3,885
Hii ni meseji iliyongia kwenye simu rafiki yangu leo asubuhi kutoka kwa mke wake mtarajiwa. Rafiki haelewi alichomfanyia mpaka amefikia hatua hiyo. Sasa jamaa anajiuliza huyu mchumba wake anamtega aili aone jamaa atafanya nini au mchumba wake tayari ana mwanaume mwingine. Amejaribu kumpigia simu simu yake haipokelewi na amejaribu sasa hivi simu haipatikani. Kwa kweli jamaa jasho linamtoka kwelikweli
 
Ha ha ha pengine mdada kakosea no,haikuwa ya rafiki yako,au walikuwa wameongea kabla ya hyo sms?
 
Sasa kama ni mchumba, hilo neno "Ukome kuniita mimi mkeo" limetoka wapi? nadhani huyo mchumba atakuwa alikusudia kumtumia mume wake wa zamani waliotalikiana, maana mtu hawezi kujiita mke wa mtu fulani pasipo ndoa, nijuavyo mimi. Othewise atabaki kuwa mchumba au mke mtarajiwa tu. Inawezekana itakuw aimetumwa wrong number.
 
Ha ha ha pengine mdada kakosea no,haikuwa ya rafiki yako,au walikuwa wameongea kabla ya hyo sms?

Nimejaribu kumuuliza amesema imetumwa kwa jina la huyo mke wake mtarajiwa hapo ndipo anapodata
 
Kumbe balazuri nilifikiri kaitwa "baladhuli"

Hizo msg sio za kujibu pengine huyo binti kakosea wrong number
 
Kwanza ajaribu kumtafuta mchumba wake amuarifu kuwa ameipokea meseji yake. Unajua simu inaweza kuwa imeibiwa,mwizi ndie katuma hiyo meseji. Pia kuna kukusea namba hapo anasema ukome kuniita mkeo badala ya mchumba huoni tatizo hapo?

Baada ya kukutana iwapo atakiri yeye ndie kaituma basi ni muhimu kwa upole aulize kulikoni? sababu gani ya kuvunja uchumba?
Si jambo zuri kuvunja uhusiano kirahisi matokeo yake utakuwa na wachumba wengi sana.
 
Mwambie atulize nafsi yake asipaparike sms katumiwa yeye lazima alotuma sms atakua na maelezo.
 
Aliyejibu ni bwana mwingine aliyekuwa anamla uroda huyo dem na sio yeye.
 
message si yake hiyo, hapokei kwa sababu bado anatafuta sababu ya kumwambia keshastuka kuwa message katuma kwingine.
 
  • Thanks
Reactions: Sal
Anapata kihoro cha nini, asubiri aonane naye ana kwa ana amuulize kuh hiyo sms
 
hiyo message ni yake na habari ndio hiyo....mwambie ajikusanye upya......
 
This world is full of wonders! Unajua najiulizaga, why Mungu alipoona kuwa-control adamu na hawa tu imekuwa issue, asingewapa simba kitoweo na human race ikaishia hapo?! What made Him think tukikombolewa tu kwa damu tutafaa kwa matumizi ya ufalme?
Sorry, tunajadili nini vilee?
 
Binti anatafuta uongo wa kumpa jamaa sio maana amelikoroga msg ya mtu mwengine kamtumia mwengine, kuweni makini sana na hizo msg za simu
 
hahahaaa nadhani atakua amepata ujumbe, hapo hamna cha mistake message imemfikia muhusika
 
This world is full of wonders! Unajua najiulizaga, why Mungu alipoona kuwa-control adamu na hawa tu imekuwa issue, asingewapa simba kitoweo na human race ikaishia hapo?! What made Him think tukikombolewa tu kwa damu tutafaa kwa matumizi ya ufalme?
Sorry, tunajadili nini vilee?

ha ha....tungeliwa na simba tungekosa senema siku hadi siku....
hapa tunajadili hivi.....mtu kapewa ujumbe hataki kuukubali.......
analazimisha ukweli uwe uwongo....

For sure huyo ameshapata mwingine, kwenye mapenzi hakuna utani wa kipuuzi kama huo, utani wa kutishiana kuachana ndio utani gani huo?
 
Limewahi kutokea kama hilo, itakuwa jamaa wa zamani kapata habari kachukua simu na kuandika sms ili kuharibu tu. Cha maana ni kumtafuta kwa kwenda kumuona na kujua kulikoni. Akijua kuwa ni jamaa wa kale amsamehe mchumba waendelee na mipango yao ya ndoa, kumbuka kuachwa na mpenzi sio mchezo, lolote atafanya kuharibu uhusiano
 
Sasa kama ni mchumba, hilo neno "Ukome kuniita mimi mkeo" limetoka wapi? nadhani huyo mchumba atakuwa alikusudia kumtumia mume wake wa zamani waliotalikiana, maana mtu hawezi kujiita mke wa mtu fulani pasipo ndoa, nijuavyo mimi. Othewise atabaki kuwa mchumba au mke mtarajiwa tu. Inawezekana itakuw aimetumwa wrong number.

Kunatitle za my huby and wiffy even before marriages now days. Uliza vijana watakwambia
 
Back
Top Bottom