Ukomo wa Rais wa Tanzania na Zanzibar ulipangwa au nasibu?

Ukomo wa Rais wa Tanzania na Zanzibar ulipangwa au nasibu?

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,507
Katika mazingira na suala muhimu ambalo linaisaidia sana CCM kuendelea kuwa madarakani ni ukomo wa Rais wa Tanzania na Rais wa Zanzibar kutokuisha mwaka mmoja/wakati mmoja kwa pamoja.

Ni ukweli kuwa ni vigumu sana katika chaguzi zetu za nchi za Afrika kuweza kumuondoa madarakani Rais anayetetea kiti chake kutokana na rasilimali na nguvu za kiutawala alizonazo. Mifumo katika nchi za Kiafrika imejengwa kuanzia juu kushuka chini badala ya kuanzia chini kwenda juu. Ndio maana Rais akiwa dhaifu hata uongozi wote nchini unakuwa dhaifu and vice versa.

Kwa nchi kama Tanzania inakuwa ni vigumu zaidi kumuondoa madarakani Rais anayetetea kiti chake kutokana na mzizi uliotokana na vyombo vya dola kufungamanishwa na siasa baada ya jaribio la kuipundua serikali ya Mwl. Nyerere mwezi Januari, 1964.

Kwa kujua jinsi ambavyo ni vigumu kumuondoa Rais Madarakani kutokana na mfumo alioasisi, Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ''upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM'. Hii ina maana kuwa mnyukano wa kweli utakuwa ndani ya CCM kabla ya kupata kiongozi mpya.

Ni wakati tu ambapo Rais aliyeko madarakani anamaliza muda wake ndio ambapo kuna uwezekano mkubwa kwa wapinzani kushinda kiti cha Rais wa Tanzania au Rais wa Zanzibar kama ilivyotokea mwaka 1995, 2015 kwa Tanzania na pia mwaka 2000 na 2010 kwa Zanzibar.

Ninaamini uwezekano wa chama tawala kushindwa ungekuwa ni mkubwa zaidi kama Rais wa Tanzania na Rais wa Zanzibar wangemaliza muhula wao wa mwisho kwa wakati mmoja.

Ni ukweli kuwa zoezi la kumpata mgombea Urais ndani ya CCM huidhoofisha sana CCM kutokana na mnyukano wa wanachama ndani ya CCM ambapo hata vyombo vya dola hugawanyika na kudhoofu.

Ukiangalia kwa sasa mnyukano umeanza huko Zanzibar kwa sababu Rais wa sasa wa Zanzibar atamaliza muhura wake wa mwisho mwaka 2020. Mnyukano huu utaidhoofisha CCM kwa upande wa Zanzibar. Juzi tumemsikia Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu akirusha ‘’vijembe’’ kwa watu waliokuwa wanadhani anaandaliwa ndani ya CCM kuwa mgombea Urais wa Zanzibar.

Athari za kudhoofu kwa CCM zinakuwa sio kubwa sana kwa sababu upande mmoja wa Muungano unakuwa na Uchaguzi wa Rais anayetetea kiti chake akifungamanishwa na vyombo vya dola. Kuachiana huku kunaifanya CCM iponye haraka makovu ya mnyukano wa ndani ya chama kabla ya kikomo kingine cha Rais wa upande mwingine wa Muungano. Hii ina maana kuwa nguvu za CCM na vyombo vya dola zinaelekezwa kule ambako kuna mgombea mpya wa kiti cha Urais.

Kwa sasa kazi iliyoko mbele ya CCM ni kupata mgombea Urais wa Zanzibar na kuhakikisha anashinda au kushindishwa!

Mipango kama hii inanifanya nijiulize kama ilitokea kwa nasibu au ilipangwa kuhakikisha CCM inavuka vikwazo vya kisiasa katika chaguzi bila kuwa na changamoto kubwa.

Ninakumbuka Maalim Seif aliwahi kusema, CCM ni dubwasha lililoota mizizi na ili kuliondoa inabidi wapinzani watumie maarifa ya kiwango cha juu.

LINK>>Maalim Seif: CCM ni dubwasha lililoota mizizi

Kama mipango hii ilipagwa basi wale wanaodhani na kujiaminisha kuwa CCM hawana fikra kubwa watakuwa wao ni wajinga au hawana fikra kubwa!
 
Magufuli atosha kwa miaka mingi aipeleke Tanzania uchumi wa kati
 
Back
Top Bottom