Ukomo wa uenyekiti Chadema ni tofauti na ukomo wa Urais Tanzania

Ukomo wa uenyekiti Chadema ni tofauti na ukomo wa Urais Tanzania

Joined
Oct 5, 2015
Posts
90
Reaction score
483
Kuna vijana wanajadili kuhusu ukomo wa uwenyekiti wa Mh. Mbowe ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) halafu wanahusisha na ukomo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wanadai kwamba kitendo cha baadhi ya vijana wa Chadema kutaka Mbowe aendelee basi kinawapunguzia nguvu ya kuwapinga vijana wa CCM wanaotaka Rais Magufuli aendelee kuongoza kwa miaka mingi.

Nadhani kuna tatizo kwenye kufikiri, au labda mimi ndio nina tatizo.

Hatupaswi kujifunza upya kwamba Demokrasia ni kuchagua. Suala la uwenyekiti wa Chadema ni suala la Chadema na suala la Urais wa Tanzania ni suala la watanzania - sio suala la CCM.

Kama wanaCCM wanaona Magufuli anafaa sana kuwa kiongozi basi waanze kupambana awe mwenykiti wao wa kudumu, kwa sababu Urais sio suala la CCM bali ni suala la watanzania wote.

Demokrasia ni kuchagua. Wanachadema wanapochagua mwenyekiti wao awaongoze kwa vipindi vinne kwa kuona inafaa, haiwaondolei haki ya kumkataa Rais wa nchi yao ambaye wanaona hafai kuongoza nchi yao.

Kama wanachama wa Chadema wameona Mbowe anafaa kuwa Mwenyekiti kwa muda wa miaka 20 au 30 haina maana kuwa na Rais Magufuli naye anafaa kuongoza nchi kwa miaka 20 au 30, na wala haina maana kuwa Rais hafai kuongoza kwa vipindi hivyo.

Endapo watanzania (sio wanaCCM) wataona inafaa Rais Magufuli kuongoza miaka 20 au 30 au zaidi, hakuna shida. Jambo la msingi ni watu kuchagua kwa hiari yao na kwa haki.

Na hata Chadema wakishika hatamu ya kuongiza nchi, hawatakuwa na uhalali wa kutaka Rais wa nchi aongoza vipindi tofauti na matakwa ya kikatiba.

Labda nisisitize hapo kwenye Urais, ni suala la watanzania na sio suala la CCM. Yeyote anayedhani suala la Urais wa Tanzania ni suala la CCM huyo ni mpumbavu mkubwa (I'm sorry my soul).

Kumekuwa na wenyeviti wangapi wa vyama vya siasa waliodumu kwa miaka mingi kuliko mwenyekiti wa Chadema?

Lipumba ni m/kiti wa CUF tangu 1995 hadi 2005, na sasa amerudi kuwa Mwenyekiti tena.

James Mbatia ni m/kiti wa NCCR-Mageuzi tangu 2000 hadi sasa, Agustino Mrema ni m/kiti wa TLP tangu 1999 hadi leo, na wengine wapo.

Sasa kwanini Chadema na Mbowe ndio iwe kisingizio?

Vijana wa CCM, na wapambe wao wa vyama vingine mnaotumia maamuzi ya Chadema kuongozwa na Mbowe miaka 20 kama kisingizio au kihalalishi cha Rais Magufuli kuomhoza zaidi ya ukomo wa kikatiba, mjitafakari.

Kama wanaona Rais Magufuli anafaa kuongoza hata miaka 100, basi kuwe na sababu za maana zinazoonesha anafaa kweli.

Na huo ni mchakato wa kitaifa, sio mchakato wa CCM na wala sio mchakato wa kuikomoa Chadema. Kuna wananchi wengi zaidi wasio na vyama kuliko wenye vyama, hao wananchi wasio na vyama hawana wenyeviti wa vyama, wana Rais wa Tanzania.

Kwa hiyo suala la ukomo wa Urais sio la CCM, sio la Chadema wala kundi fulani, ni suala la Watanzania wote.

Kama CCM wanaona wivu Mbowe kuongoza Chadema miaka 20 na wao wafanye mchakato Magufuli awe Mwenyekiti wao kwa miaka wanayoyaka.

Lakini pia nitoe angalizo kwa watu wanaofikiri kuondoa ukomo wa Rais Magufuli, kuna mambo ambayo si ya kujadili hadharani lakini ni vema kutoa angalizo. Kama nilivyosema awali, Rais sio wa kundi fulani, ni Rais wa nchi ambaye maamuzi yake na ushawishi wake unaathiri watanzania wenye itikadi tofauti, imani za dini tofauti, mitazamo tofauti.

Kuna mambo mazito yanaweza kufanya nchi iachane na mpango wa uchaguzi, mfano Marekani kwenye Demokrasia kulikuwa na mpango wa kufuta uchaguzi wa Urais wa mwaka 1988 wakati Rais Ronald Reagan akimaliza muda wake.

Sababu kubwa ilikuwa hofu ya kuvamiwa kijeshi na muungano wa Sovieti. Yapo mambo mengine yanaweza kulazimisha nchi kumuondoa kiongozi badala ya kuendelea kuwa naye, na hiyo nadhani ndilo linalohusu zaidi Tanzania.

Masuala ya Udini na Ugaidi - baadaye kidogo yanaweza kutulazimisha kubadili uongozi (Kama tuna akili). Wengine waendelee kujadili mabarabara na standard gauge.

Ni uzembe wa kufikiri' kutumia mfano wa kundi la Chadema lenye watu wa itikadi za kisiasa zinazofanana na kulinganisha na Urais wa nchi nzima.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom