Ukondefu unaninyima amani nifanyeje ili nipate walau vinyama kidogo

Ukondefu unaninyima amani nifanyeje ili nipate walau vinyama kidogo

ungeambatanisha bac japo na ka photo nyie vimbau mbau ndio ugonywa wangu ajabu ss nikimpta kimbau mbau anakuwa chibonge baada ya muda
 
Oy mi mwanaume makalio ya nini sasa mbona unaleta mizaha katika issue seteous ndugu
Hii huduma ni optional kama utapenda kunenepeshwa mwili ila nyuma ubaki flat is up to wewe, nimetoa tu wazo kwa kuwa mwili unapaswa kunona proportional kwa uwiano sawa!
 
kul
HABARI WAKUU.
Wakubwa kwa Wadogo salamu kwenu
Mimi ni kijana mwenye 28 years..!

Tatzo langu ni uwembamba uliopitiliza natamani walau na mimi niwe na vinyama kidogo. Nakumbuka mwaka jana niliwahi kupima uzito wangu nikawa 48kg uzito wa Jogoo la kienyeji iliniuma sana nilikaa wiki zima nikitafakari hatma ya afya yangu hadi hapo nilipoenda kupima magonjwa yote nikakutwa nipo smart sina tatzo la kiafya!

Nikaamua kujianzishia Dozi ya kula matunda kila baada ya chakula na mara kwa mara hali ambayo ilikuwa inanigalimu kila siku kutumia galama zaidi ya elfu kumi 10,000 kwa ajili ya Kuimalisha Afya yangu pia nilipata ushauri wa kula kitimoto na Bia moja kila siku! Hali ambayo sikuona shida nilikuwa nafanya hivyo hadi kujikuta nakuwa mlevi wa bia, Maana nilikuwa nakunywa bia moja kwa ajili ya Afya ila hatmae nikajikuta nakunywa bia zaidi ya 5 kwa siku maana tabia ya Bia nilikuwa nikinywa moja natamani kuongeza nyingine na nyingine hadi nikajikuta nakuwa mlevi pasipo kukusudia hali hii ilikuwa inanipelekea kukosana na watu wanaonizunguka kila nikinywa pombe nawatambia majirani zangu kuwa hawana hela na kusababisha fujo hadi nyumbani kwangu! Ikabidi nijishauri mwenyewe nakuacha dozi hii kwa sasa situmii tena.

Ila katika kumbukumbu zangu kipindi nafanya haya walau nilianza kuona mabadiliko kidogo ya afya mwilini mwangu nikaanza kutokeza kakitambi kwa mbali na kunenepa shavu na nilipopimwa uzito nilikuwa nimefikisha 60Kg hadi watu walianza kuniambia nimenenepa pasipokujua hiyo hali inaniingiza galama kiasi gani!

Nilikuwa nimeanza kunyanyua kakibanda kangu ila nilisimamisha shughuli ya ujenzi, pesa yote niliokuwa napata katika mihangaiko yangu ikawa inatumika kwa ajili ya kufanyia kile ninachokitamani, baada ya kuacha tena dozi hii kwa sasa nimepururuka vibaya mno jana nimepima uzito nakuta 52kg tu na kila kukicha nazidi kukonda tena!

Nimeamua kuja hapa ili wataalamu mnipe namna ambayo itakuwa si ghali sana ambayo nitatumia ili ninenepe huu ukondefu unaninyima michongo mingi sana!
Atakaeweza kunisaidia nipo tayari kumlipa!
kula bia kwa wingi mkuu
 
Mimi huyoo
Screenshot_20190805-122743.jpeg
 
1. Mimi si daktari
2. Beer moja tu na chakula mchana na jioni. Kama uko kazini jioni tu.

Ukinywa beer na chakula ina kucontrol kuongeza. Ikiwezekana nunua unywee nyumbani.

Wewe ni daktari nakufahamu vizuri 📢 na kesho tukijaliwa ntapitisha kuku pale nyumbani..
Asante kwa ushauri mkuu hebu namimi niufanyie kazi ntaleta mrejesho hapa
 
ungeambatanisha bac japo na ka photo nyie vimbau mbau ndio ugonywa wangu ajabu ss nikimpta kimbau mbau anakuwa chibonge baada ya muda

Unakwama wapi sasa wakati wakati mimi nipo na sixpack zake
 
We kula vitu vya sukari na mafuta tu ila nyama ndio nzuri kwa kujaza misuli. Hakikisha hukosi bakuli ya supu ya ng'ombe deile.

Mchana ugali na nyama ya kitimoto roast.

Jioni kuku choma na chips zitakufaa sana mkuu. Huku ukisindikizia na malta.

Nakupa mwezi na nusu tu, ulete majibu hapa.
 
Ukila matunda inamaana unabalance diet huwezi kunenepa bali utakonda zaidi.
Kunenepa ni kuharibu mfumo
Cha kufanya kula kila kinachonenepesha
Asubuhi kula kiporo cha wali.. mchana ugali mkubwa mboga 7 shushia na soda.. usiku chips/wali/ Nyama na juice ya kutengeneza
Ukipita njiani usisahau kula vitu vidogo vidogo/ michemsho nk
Yani kula iwe first priority
Kikubwa na mno usiwe na mawazo
 
We kula vitu vya sukari na mafuta tu ila nyama ndio nzuri kwa kujaza misuli. Hakikisha hukosi bakuli ya supu ya ng'ombe deile.

Mchana ugali na nyama ya kitimoto roast.

Jioni kuku choma na chips zitakufaa sana mkuu. Huku ukisindikizia na malta.

Nakupa mwezi na nusu tu, ulete majibu hapa.

Huyu sharobaro ataweza kusindilia nyama kweli zaidi ya mishkaki minne
 
Acha gubu,penda kuish bila karaha,acha mawazo ya kifala fala,pata muda wa kupumzika,rizika unachopata, kula diet stahk,fanya mazoez ya kuongeza weight,HAKIKA mwili huo miez 2 mingi utambi huo unakuja
 
Back
Top Bottom