Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Consultant

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2008
Posts
11,503
Reaction score
20,892
Rafiki yangu mmoja nilimkopa Laki Sita May 2017. Alikuwa nje ya mji na mkewe akapata emergency, akihitaji hiyo pesa. Kwa kuthamini urafiki wetu, nilimtumia fasta, na elfu kumi juu ya ''kutolea''. Huyu hajalipa mpaka leo. Mwingine alikuwa staff member na akaomba nimkope Laki Nane kwa kuwa alikuwa na shida ya kutoa kagari kake kapya bandarini. Ilikuwa June mwaka jana. Hajalipa mpaka leo.

Jambo la ajabu sasa, naona kama urafiki wetu umetetereka pakubwa sana kwa wote wawili. Sio kwamba nawasumbua kwa kuwadai, la hasha. Naona mmoja yeye hata nikichat nae, ule ukaribu wetu wa zamani haupo tena. Sasa hivi simuoni kabisa WhatsApp na nimeambiwa kabadilisha namba. Huyu wa Laki nane zaidi ya mara mbili amepokea simu zangu na kusema ''nipo busy/meeting mkuu, ntakucheki baadae buddaaa...''. Hakunicheki mpaka kesho kutwa. Last time nilitaka kumpa mchongo wa kazi moja hivi lakini alivyoyeyusha, deal nimempa mwingine.

Anyway, kopa mtu fedha at your own risk. Kwa kuwa ninathamimi sana urafiki, mwaka huu sintomkopa fedha mtu au rafiki yangu yeyote. Kama ni fedha kidogo na nimesukumwa na shida ya mtu, nitatoa msaada bure na halitakuwa deni. As for the two gentlemen, nimeshawasamehe moyoni ila sitawaambia na itakaa iwatese tu.
 
Yaani ''tunaachana'' kwa hela kiduchu hivi....inasikitisha.
Hiyo sio hela kiduchu, ni nyingi sana kama umebanwa mbavu. Cha msingi unachotakiwa kujua ni kwamba hao hawakuwa marafiki bali ni watu mliotokea kujuana nao sana na wewe ukadhani ni marafiki.

Wangekuwa marafiki, wangekushirikisha changamoto zao bila aibu.
 
Mkuu nikopeshe laki 5 ntakulipa next week
 
Mkuu usiseme hvyoo,,,,kuna mtu atakukopa utakua huna namna ya kumnyma
 
Nimepita katika matukio kama yako Davis nilimkopesha pesa ndefu ya kumlipia mwanae ada kuna kipindi alisitishiwa mshahara hajanilipa hadi leo.Ally nae hivyo hivyo ila nimewagundua kuwa sio marafiki wa kweli na sitawadai
 
Kuna ndugu yangu alikua na roho ngumu sana, yeye hataki kusikia neno NIKOPESHE. Ukimuomba laki anakupa elfu10 halafu anakwambia nimekupa tu sitokudai. Unajua kwenye maisha unatakiwa bandidu sometimes.
 
Mimi nimekoma kukopesha mtu sitaki kabisaaaa....Kuna watu hata aje aniambie anashida kubwa kiasi gani sitampa labda nitoe sadaka kiasi ninachojiskia mm na sio kile alichoomba.
Na kitu kimoja ni watu kukosa uaminjfu anasema ntakupa j3 ijajayo ikifika hiyo siku hapatikani au yuko bussy. Hawajui ni kiasi gani wanakukwamisha .Mbaya zaidi mi mtu akigoma kulipa nwambia ndugu wakati nakupa hiyo pesa sio kwamba nilikua sina kazi nayo ila tu nilithamini shida yako kwanza.
Sijui kwanini, yani sijui kwanini watu sio waaminifu wanapokopa.
Mimi nimejiwekea kutokupenda kukopa na ikitokea nakopa nalipa kwa wakati kama nilivyo ahidi na nikishindwa siku niliyoahidi namjulisha mhusika mapema aniongezee siku kadhaa lakini lazima nilipe.
Sipendi watu wasiolipa madeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…