Consultant
JF-Expert Member
- Jun 15, 2008
- 11,503
- 20,892
Rafiki yangu mmoja nilimkopa Laki Sita May 2017. Alikuwa nje ya mji na mkewe akapata emergency, akihitaji hiyo pesa. Kwa kuthamini urafiki wetu, nilimtumia fasta, na elfu kumi juu ya ''kutolea''. Huyu hajalipa mpaka leo. Mwingine alikuwa staff member na akaomba nimkope Laki Nane kwa kuwa alikuwa na shida ya kutoa kagari kake kapya bandarini. Ilikuwa June mwaka jana. Hajalipa mpaka leo.
Jambo la ajabu sasa, naona kama urafiki wetu umetetereka pakubwa sana kwa wote wawili. Sio kwamba nawasumbua kwa kuwadai, la hasha. Naona mmoja yeye hata nikichat nae, ule ukaribu wetu wa zamani haupo tena. Sasa hivi simuoni kabisa WhatsApp na nimeambiwa kabadilisha namba. Huyu wa Laki nane zaidi ya mara mbili amepokea simu zangu na kusema ''nipo busy/meeting mkuu, ntakucheki baadae buddaaa...''. Hakunicheki mpaka kesho kutwa. Last time nilitaka kumpa mchongo wa kazi moja hivi lakini alivyoyeyusha, deal nimempa mwingine.
Anyway, kopa mtu fedha at your own risk. Kwa kuwa ninathamimi sana urafiki, mwaka huu sintomkopa fedha mtu au rafiki yangu yeyote. Kama ni fedha kidogo na nimesukumwa na shida ya mtu, nitatoa msaada bure na halitakuwa deni. As for the two gentlemen, nimeshawasamehe moyoni ila sitawaambia na itakaa iwatese tu.