Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Jamaa yangu aliniomba mkopo wa laki mbili.Nikamuahidi nitampa nikizipata.Akawa ananipigia simu mfululizo kunikumbusha na ahadi za kulipa ndani ya mwezi.Nikaja kumpa.Huu ni mwezi wa tano hajalipa.Najuta sana.
 
Nikimkopesha mtu siku hizi namuuliza kabisa na ukishindwa kurudisha option B ni nini kama ni simu, laptop au chochote cha thamani ya ile hela. Wengi wakikopeshwa hawarudishi. Kuna rafiki yangu mkaka tulisoma wote nilimkopesha laki akasema atarudisha ila akachuna kila nikipiga simu hazipokelewi wala sms hajibu. Ilikuwa 2016 mwaka jana July akatuma sms ya kuomba mchango wa harusi anaoa nikamjibu "ndugu mchango wangu unao we niletee kadi ya mwaliko nije " ndo kimya hadi leo.
 
Mi nakopesha jamani kwa riba, kiwango kuanzia 1m - 20m

Karibuni
 
Yaani ''tunaachana'' kwa hela kiduchu hivi....inasikitisha.
Heri wewe ni rafiki huku ni ndugu, yaani ukitaka kuonekana mbaya dai chako!
Dawa ni kuithamini Pesa kama mtu maana Pesa ina personality, inamfuata mtu anae mpenda!
Shkamoo Pesa!
 
These were close buddies...tunakunywa pamoja. Nasikitika urafiki wanauvunja kindezi hivi...
Achana nao
Hao wana roho za umaskini
Tena usipoangalia watakuambukiza pepo la umaskini
Piga chini hiyo mijitu
 
Ukitaka kuua urafiki na mtu,hasa muafrika,mkopeshe pesa.
 
Daah unanikumbusha machungu mzee....nimekopesha rafiki zangu wawili mil 6 mwaka jana january, mpaka leo mwaka umeisha holaaa na urafiki wetu upo mashakani. Nimeshahesabu maumivu ila nimeamini usimkopeshe ndugu au rafiki pesa mpaka roho mtakatifu akushukie, labda uamue kutoa kama msaada tu.
 
Back
Top Bottom