Ukosefu wa ajira na umasikini unasababishwa na viongozi wa serikali wasio kuwa na maono

Mzee wa old school

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
873
Reaction score
1,405
Bila shaka mu wazima kabisa.

Leo katika mizunguko yangu ya kusaka tonge,, nimepita barabara ya g/mboto... Nimeona wameanza Ujenzi wa barabara na vituo vya magari ya mwendo kasi,, wakati gari imesimama kwenye foleni nimetafakari mengi sana...

1. Nimeona wakandarasi wa kichina, hivi kwanini serikali isitoe tenda ya kandarasi KWa kampuni za Tanzania? Lengo pesa zisitoke nje ya tz mzunguko uwe hapa KWa asilimia zote. Sawaaa mchina ataajiri watanzania... Lakini si vibarua tu? Kwahiyo pesa nyingi itarudi kwao.

2.nikawaza labda watasingizia hakuna watalaam. Sawa hakuna. Kwanini wasiwatengeneze hao watalaam? Heri gharama itumike kuwatengeneza ili iepushe hasara kubwa ya badae.

3. Nikawaza tarura na tanroad,,, kazi yao kubwa nini,,,, maana tenda zote wachina wamezichukua,, kama sio kampuni ya mchina basi ni mzungu ama mturuki ama yeyote kutoka nje ya bara la afrika. Shida ni nini?

KWa kweli imeniuma sana.... Hebu watumie hata wanajeshi basi kama wakiona namna gani.
 
Wewe unajua watanzania kweli??? Hamna mtanzania anae weza kazi zamaana, tuna kasoro nyingi, kazi tunazo weza ni za udalali tu kwasbb msingi yake ni maneno mengi na uongo uongo ila kazi zingine thubutu
Ni kweli.... Wa Tanzania wengi kupiga domo ndo dili, kujipendekeza, mara kujiita machawa wa mazaa.... Ili tu wateuliwe waendelee kupiga domo maisha yaende...

Lakini nafasi ipo.... Tukuze watoto wetu katika misingi ya kazi na si maneno....
Tuwaambie maneno hayapeleki chakula mdomoni isipokuwa mkono...
 
Chuki iliyoko vifuani mwa unemployed youths.. Ni nyuklia inayotokota. Picha nzuri ni wakati ule wa sensa vijana walivyojitokeza mpka maafisa kata wakabaki mdomo wazi. Wengine wakasema hawakujua kama kata yao inawasomi kiasi kile.

Yaipasa serikali kuchukua hatua ya haraka na kuacha kulinganisha jambo hilo na nchi zote duniani. Maana kila nchi ina resources ilizoumbiwa na M/Mungu.

Pia hili limechangia muamko wa elimu kushuka ama kufa ndio sababu watoto wanaona hawana sababu ya kwenda sekondary. Bora wakafanye biashara mbalimbali mapema.
 
Unachosema ni kweli kabisa
 
Kabsa.nimaumiv kwel hasa ukiwa umetoka familia za kimaskin na hali ii ya uchumi.
 
Back
Top Bottom