Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Tujifunze kusoma fani zinazotuachia ujuzi ili tuweze kujiajiri na pia kutengeneza ajira kwa wengine. Mfano mdogo tu, jaribu kutangaza nafasi ya fundi wa kushona mavazi; inaweza kuchukua wiki, miezi hakuna mtu aliyeomba. Hii inatafsiri, wenye hiyo fani wako bize na mambo yao na hawaitaji kuajiriwa.
Sasa, jaribu kutangaza nafasi za afisa rasilimali watu, wachumi, wahasibu, wanatakwimu, wagavi, ustawi wa jamii, wanasheria, waalimu n.k utashangaa ndani ya muda mfupi watu zaidi hata ya 1000 hata wenye PhD wataomba, ingawa nafasi ni moja tu; hii inatafsiri elimu waliyoipata haijawawezesha kujikomboa.
Kinachotakiwa ni jitihada binafsi, kujifunza kitu kitakachokutambulisha wewe ni nani, na una uwezo upi wa kujitengenezea ajira pamoja na kutengeneza ajiri kwa wengine.
Bado hatujachelewa, muda ni sasa.