LugaMika
Member
- Mar 13, 2024
- 38
- 53
Wazazi wanatuombea sana hususa wale wa familia za chini pale wanapoona kijana au Binti yao yupo chuoni, kwani imani yao atapata Elimu kisha kuwa na maisha bora.
Lakini tatizo vuoni kunakuwa na mipango malidhawa ya Wakufunzi kukwamisha ndoto za vijana au Mabinti hawa. Tupia mbali rushwa kwani ni tatizo ambalo lipo na inaaminika halikomi kulingana na tamaa zilizopo.
Lakini kuna hili nalo linazidi kukuwa kwa kasi hasa kwa ndaki za uhandisi.
Kuna Wakufunzi hu dhamimini kozi fupi ambazo mara nyingi huhusiana na kozi ambazo hutakiwa zifundishwe darasani. Na kozi hizi hutoza fedha na pia hufanyika wakati wa likizo. Sio vibaya kuanzisha vitega uchumi vya namna hiyo vyuoni.
Lakini ubaya unaanza pale ambapo itafika muda wa masomo na anahitajika afundishe darasani lakini yeye akasema hii sitofundisha sana kwakuwa baadhi yenu walisoma kama kozi fupi wakati wa likizo kwahiyo mtawauliza.
Kauli hii ni moja kati ya maneno ya kibaguzi na unyonyaji wa wazi wazi.
Kutokana na changamoto hii kama hiitofuatiliwa tunaweza kuzali Wahandisi wasio na weredi kabisa .
Mimi pia ni muhanga wa mambo ya namna hiyo.Je, hili suala nilipeleke wapi ili liondolewe?