Malyenge
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 6,658
- 3,659
Kwa muda mrefu sasa imekuwa nikisikia wazazi na wanafunzi wakilalamikia kufanya vibaya katika mitihani ya masomo ya sayansi. Mojawapo ya sababu ya kutofanya vizuri wamekuwa wakisema ni kutokuwa na maabara........
Kwamba kama kungalikuwapo maabara na vifaa na walimu wa kuzisimamia maabara hizo wanadai kwamba wangeliweza kufanya vizuri sana katika masomo ya sayansi......Huo ndio ukweli siku zote nimekuwa nausikia miaka yote hadi na mimi nimekuwa mtu mzima leo hii lakini ukosefu wa maabara na vifaa umekuwa ni wimbo usiokuwa na mwisho.
Nimekuwa nikifuatilia sana jambo hili kujua ukweli wake na nimekuwa nikijiuliza sana maswali yafuatayo:
1.Ni asilimia ngapi ya maksi zinahusisha elimu ya maabara katika masomo ya sayansi
2. kwamba je ni topic zote katika masomo ya Kemia, Biolojia na Fizikia zinahusu maabara tu???
3. Je somo la hisabati nalo linahitaji maabara? Ama hisabati siyo sayansi? Maana nalo watu wengi wanafeli sana......
Nikafanya utafiti wa maswli hayo kisha nikaja na majibu yafuatayo:
1. Kwamba huwezi kwenda maabara kwanza mpaka usome nadharia (theories)
2. Nadharia ndo inapelekea ukienda maabara uweze kujua unafanya nini
3. Hakuna topic inayojitegemea ya kuhusu maabara bali topic zote zimo humohumo unamosomea nadharia
4. Kwa hiyo ukijua nadharia asilimia miamoja na elimiu ya vitendo ukiwa maabara unajua asilimia miamoja
5. Kwa kulijua hilo serikali iliweka mtihani wa bila maabara kama mbadala wa mtihani wa maabara (yaani alternative to practical)
Kutokana na utafiti wangu na majibu kama mlivyoyaona hapo juu ukapelekea mimi kuja na maswali yafuatayo:
1. Kwa nini somo la hisabati halihusishi maabara lakini bado watu wanafeli?
2.Kwa zile topic zisizohusisha maabara wanafunzi huwa wanapata maksi ngapi ili tuone kinachosababisha wafeli?
3. Kama maabara ni sehemu ya elimu ya nadharia kwa nini watu wanaona elimu ya vitendo ndo inawakwamisha?
4. Kama kulalamikia ukosefu wa maabara na elimu ya vitendo madaktari ndo wangelalamika zaidi maana wao ndo wanahitaji maabara kuliko mtu yeyote. Mbona madaktari wako vizuri inakuwaje kama maabara pekee ndo inamfikisha mtu mbali imekuwaje msingi wa kukosa elimu ya maabara usiathiri elimu ya madaktari huko mbele wakiendelea?
5. Kama elimu ya maabara ni kikwazo na yale masomo mengine kama vile General Studies mbona na yenyewe wanafeli?
6. Somo la kiswahili hata anayesoma sayansi (wa o'level) pia nalo hulisoma.....Sasa inakuwaje nalo mwanasayansi analifeli? Na lenyewe linafundishwa maabara?
Baada ya maswali hayo nikaja kuhitimisha ya kwamba sababu kubwa ya watu kulalamikia ukosefu wa maabara ya elimu hiyo ya vitendo ni kukosa juhudi binafsi badala yake ni kutafuta pa kutokea. Wanafunzi hawataki kujituma hata kwa zile topic zilizo wazi hazihitaji ufundi wowote unakuta mtu anaulizwa swali lakini anapoteza maksi eti halijui. Hizo maksi alizozikosa anazihamishia kwenye practical kwamba ndo imemfelisha.
Utakuta mtu wa ordinary Level anashindwa kufaulu somo la civics ama history sasa kama yule wa sayansi anasingizia maabara je na huyu aliyefeli civics na history atasingizia nini?
Tuna kazi kubwa watanzania.......