KERO Ukosefu wa maji safi na salama kwa baadhi ya kata Wilaya Bunda vijijini

KERO Ukosefu wa maji safi na salama kwa baadhi ya kata Wilaya Bunda vijijini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa kunda vijijini tunalazimika kuchota maji ziwani ambapo wanyama wananywea humo, watu wanafulia, kuogea na kuoshea vyombo ziwani.

Bado maji hayo hayo tunalazimika kutumia kwa kunywa na kupikia hasa kwa wakazi walio pembezoni na barabara ya ukerewe inayopita kibara.

Watoto wanahatari kubwa ya kuliwa na mamba wanapoenda ziwani. Mamlaka zipo kimya.

Tunamuomba waziri wa Maji
Jumaa Aweso atembelee maeneo yetu na kutatua changamoto. Mbunge pia atusemee bungeni tutapata kipindupindu kwa hii hali.

Watumishi hawakai sababu ya hizi changamoto na vyombo vya habari havitusemei.

Waziri mkuu ziara yako mkoani Mara tunaomba ilete manufaa kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom